Skip to main content

Posts

Showing posts from 2020

Afya Ya Kinywa na Meno kwa Watoto

MAGEGO YA MWISHO - (WISDOM TEETH)

       Magego ya mwisho au wisdom teeth ni meno ya mwisho kabisa kuota katika mdomo na huota kati ya miaka 17 mpaka 25. Meno haya huwa  mawili kwa kila taya  moja kila upande wa taya na kufanya jumla yake iwe manne. Sio watu wote huota haya magego ya mwisho na hata kam yakiota kwa watu wengi huwa hayajakaa katika mstari kama meno mengine lakini kwa wachache huwa yanaota vizuri kabisa. Mara nyingi magego ya mwisho huotea ndani ya taya na hayatoki nje na hata kama yakitoka huota vibaya na kusababisha kuoza na hata magonjwa ya fizi hii husababishwa na kuwepo kwa fizi juu ya meno haya ambayo huifadhi vyakula na kusababisha infection na maumivu. Kwanini magego ya mwisho huota vibaya? Magego ya mwisho huota vibaya kwasababu hayapati nafasi ya kuota kwa kawaida. Magego ya mwisho huota kati ya miaka 17 mpaka 25, umri ambao mdomo tayari unakua na meno mengi hivyo basi kukosa nafasi ya kuota vizuri na kuishia kuota katika hali ambayo sio ya kawaida (impacted)....

WASIWASI WA MATIBABU YA MENO: NJIA 3 ZA KUSAIDIA KUONDOA WASIWASI WA MATIBABU

              Kama umekua ukipata wasiwasi wa kwenda kumuona daktari wa meno, jua kwamba hauko peke yako. Pengine unahisi utapata maumivu au hujui nini daktari atafanya kulingana na atakachokiona. Sababu za wasiwasi zinaweza kuwa; Kutokuwa na taarifa sahihi kutoka kwa daktari, kupata maumivu baada ya matibabu au mawazo hasi kuhusu matibabu ya meno. Kwa sababu yoyote ile, timu nzuri ya madaktari itasaidia kuhakikisha afya yako ya kinywa na meno pamoja na kimawazo inakuwa nzuri. Unavyochelewa zaidi kumuona daktari wa meno ndivyo unavyokua kwenye hatari ya kupata matatizo makubwa zaidi na kusababisha matibabu yawe magumu zaidi. Mathalani, kumuona daktari wa meno mapema kutasaidia kufanya matibabu yawe rahisi na muda mfupi. Zifuatazo ni njia ambazo unaweza kuzitumia ukiwa unaenda kumuona daktari wa meno ili kupunguza wasiwasi na kufanya uwe na tabasamu lenye uangavu. Ongea Mtu yoyote mwenye wasiwasi, akiongea hufanya mabadiliko makubwa kwa hisi...

MAFUA NA KIKOHOZI; MAMBO MATANO UNAYOPASWA KUFANYA UKIWA NA MAFUA NA KIKOHOZI

        Ukiwa na mafua na au kikohozi, kuweka mwili wako sawa na katika hali ya usafi ni jambo la msingi na muhimu na hii inahusisha usafi wa kinywa pia. Zifuatazo ni njia rahisi ambazo unaweza kuzitumia ili kuhakikisha afya ya kinywa na meno inabaki kuwa nzuri na imara wakati unaumwa. Zingatia Usafi mzuri Ukiwa unaumwa  mafua na kikohozi ni vyema kuziba mdomo na pua wakati wa kukohoa na kupiga chafya pia usisahau kuhakikisha afya ya kinywa chako inazingatiwa. Tafiti zinaonesha kwamba virusi vya mafua vina uwezo wa kukaa sehemu yenye unyevu kwa takribani masaa 72. Hivyo basi ni vyema kutoshirikiana kutumia mswaki mmoja kwa watu wawili pia ni vizuri kubadilisha mswaki mara baada ya kupona mafua ingawa asilimia za kupata mafua kutoka kwenye mswaki ni ndogo lakini ni vyema kuchukua tahadhari. Tumia dawa ambazo hazina sukari Kama inavyojulikana kwamba sukari ndio chanzo kikubwa cha meno kuoza, hivyo basi kutumia dawa ambazo zina sukari zinaweza kuleta at...

KUNG'ARISHA MENO (TEETH WHITENING) - VITU UNAVYOPASWA KUJUA

Kupiga mswaki kwa usahihi ndio njia ambayo inaweza kukufanya uwe na tabasamu zuri na meno yenye mng'ao. Lakini je unawaza kufanya meno yako yawe meupe zaidi? Basi ni vizuri ukajua ukweli kuhusu matibabu haya. Nitaelezea kwa kujibu maswali ambayo huwa yanaulizwa sana kuhusu kufanya meno yawe meupe. Kwanini Meno yanabadilika rangi? Kwa muda meno yako yanaweza kubadilika kutoka rangi nyeupe kwenda kwenye rangi iliyofifia kutokana na sababu tofauti ambazo ni; Vyakula na vinywaji; Kahawa, chai na mvinyo mwekundu ni vinywaji ambavyo vinaleta sana kubadilika kwa rangi ya meno. Vinywaji hivi vina rangi ambayo huganda kwenye tabaka la nje la meno. Matumizi ya tumbaku na sigara; Vitu viwili vilivyopo kwenye sigara ndivyo hufanya rangi ya meno ibadilike navyo ni lami na nicotine. Lami ni nyeusi kwa asili lakini nicotine hubadilika rangi inapochanganyika na hewa ya oxygen na kuwa njano ambayo huonekana sana kwenye meno ya wavutaji wa sigara. Umri; Chini ya tabaka gumu kabisa la meno ku...

UKWELI KUHUSU NJIA ZA ASILI ZINAZOTUMIKA KUNG'ARISHA MENO

Linapofika suala la kufanya meno yawe meupe, kuna njia nyingi ambazo zimekua zikiwekwa kwenye mitandao ya jamii na hata magazeti. Watu wengi wakiulizwa ni njia gani wanahisi wataweza kuifanya tabasamu lao liwe zuri zaidi majibu yao ni kwa kufanya meno yawe meupe zaidi. Tabasamu lenye afya huja katika njia tofauti, ingawa inatamanisha kufikiri kwamba vitu tulivyonavyo jikoni vinaweza vikawa ufumbuzi wa tabasamu zuri. Njia kuwa ya asili haimaanishi ni njia ya kiafya. Njia za kiasili zinaweza kusababisha matatizo makubwa kuliko faida ambayo unaiwaza kuipata. Zifuatazo ni baadhi ya njia ambazo watu huhisi ni sahihi lakini kiafya zina madhara katika meno yako. MAGADI (BAKING SODA) Watu hutumia mchanganyo wa magadi na tindikali zitokanazo na matunda kama machungwa na mananasi.                        Ukweli ni kwamba, kula matunda kiafya ni vizuri lakini mchanganyo wa magadi na ...

MFUNGO NA AFYA YA KINYWA NA MENO

       Watu wengi wanatokea kusahau kufanya usafi wa kinywa na meno wakiamini kuwa hakuna tatizo litawapata katika kipindi cha mfungo. Kuhakikisha usafi wa kinywa na meno utasaidia kupunguza harufu mbaya ya kinywa na kinywa kuwa kikavu. NINI HUTOKEA UKIWA UMEFUNGA? Kufunga husababisha kuongezeka kwa kampaundi za madini ya sulphur katika kinywa na husababisha harufu mbaya ya kinywa. Watu wengi wanaamini kuwa kufunga husaidia kutibu magonjwa ya fizi, hii sio kweli. Kuongezeka kwa kampaundi za madini ya sulphur huenda sambamba na kupungua kwa mtiririko wa mate katika kinywa ambayo husababisha kutengenezwa kwa matabaka ya uchafu katika meno kitu ambacho moja kwa moja hupelekea matatizo ya fizi na meno kutoboka. JINSI YA KUTUNZA AFYA YA KINYWA NA MENO KIPINDI CHA MFUNGO. Changamoto nyingi za afya ya kinywa na meno huwepo kipindi cha mfungo. Wengi wamezoea harufu mbaya ya kinywa katika kipindi cha mfungo na huwa wanahisi ni jambo la kawaida. Fanya mamb...

MATE NA MATUMIZI YAKE KATIKA KINYWA.

  Mate yana kazi kubwa na muhimu katika kuimarisha afya kinywa na meno. Hutokana na mfumo wa damu na hivyo huwa kama mkondo wa damu katika kinywa. Hii humaanisha kuwa kama ilivyo kwa damu, mate pia hufanya kazi kubwa katika kuimarisha na kulinda afya ya tishu laini na ngumu katika kinywa. Mtiririko wa mate ukipungua katika kinywa, matatizo kama kuoza kwa meno na vidonda vya mdomoni huanza kujitokeza. Kutafuna ni njia mojawapo ambayo huamsha mtiririko wa mate katika kinywa, husababisha misuli kugandamiza tezi za mate ambazo huzalisha mate. Kazi za mate ni pamoja na; Kuondoa mabaki ya vyakula yaliyoganda katika meno na fizi Kulainisha na kukivunja chakula ili kurahisisha kumeza Kusaidia kuimarisha ladha Kulinda dhidi ya maradhi yanayoweza kushambulia meno na tishu za kwenye kinywa Kufanya uso wa meno kuwa imara kwa kupakaza madini ya calcium, flouride na phosphate katika meno. Pamoja na kulinda na kuimarisha afya ya kinywa, mate yanaweza kuwa na viashiria vya afya...

MATIBABU YA KUSAFISHA MIZIZI YA MENO (ROOT CANAL)

  Kama una jino lililoharibika sana, kuoza au lenye maambukizi (infection), daktari wa meno anaweza akashauri matibabu ya kusafisha mizizi au root canal. Matibabu ya kusafisha mizizi ya jino yanatumika kuokoa jino pale inapohitajika badala ya kulitoa. Nini Hufanyika katika matibabu ya kusafisha mizizi ya jino? Jinsi jino lilivyo kwa muonekano wa ndani. Jino huwa na nafasi ndani yake ambayo huwa na mishipa ya fahamu na damu ambayo hulifanya jino liwe hai. Sehemu hii inaweza kupata maambukizi kama; Una tundu kwenye jino ambalo ni kubwa sana Matibabu ya muda mrefu ambayo yanaweza kusababisha matatizo kwa sehemu hii. Jino likivunjika au kupasuka Ajali yoyote kwenye jino Ukiwa na moja ya matatizo hayo na yasitibiwe, jino hupata maambukizi na kusababisha maumivu makali na wakati mwingine uvimbe ambao husababishwa na jipu linaloota kwenye ncha ya mzizi wa jino. Maambukizi haya yanaweza kusababisha kupoteza jino kwa sababu bacteria wanaosababisha maambukiz...

KUTOBOA MIDOMO (ORAL PIERCINGS)

Kutoboa mwili kumekua kitu maarufu siku za karibuni na imekua kama njia ya kujielezea na kujitambulisha. Kutoboa midomo kunaweza kuonekana ni kitu kizuri na cha kupendeza lakini kinaweza kuleta madhara makubwa kwa mwili na afya. Hii ni kwa sababu kinywa kina vijududu vingi sana ambavyo vinaweza kusababisha maambukizi na kuvimba hasa baada ya kutoboa sehemu za kinywa na midomo.  Kama umetoboa ulimi, mashavu, midomo (lips) na kilimi (sehemu ya nyuma kabisa ya koo), hii inaathiri sana kuongea, kutafuna na pia kumeza, vilevile inaweza ikasababisha; Maambukizi, maumivu na kuvimba. Kwa sababu ya uwingi wa bakteria katika kinywa, kutoboa sehemu za kinywa kunaweza sababisha maambukizi ambayo huwa pamoja na maumivu na kuvimba. Kuvimba kwa ulimi au sehemu aya nyuma ya koo kunaweza sababisha kukosa pumzi na hata kupoteza maisha. Kuharibika kwa meno na fizi Mzio au Allergy Kuharibika kwa mishipa ya fahamu. Hii ni hasa kwa kutoboa ulimi. kunaweza kusababisha kuharibika kwa miship...

HOMONI NA AFYA YA KINYWA NA MENO; JAMBO AMBALO KILA MWANAMKE ANAFAA KULIFAHAMU

                        Uzito, mhemko (mood) na afya ya kinywa na meno. Kuna kitu kimoja ambacho kinaendesha hivi vitu vyote, nacho ni homoni. Unaweza ukajiuliza ni vipi homoni zinauhusiano na afya ya kinywa na meno kwa mwanamke, hii ndio sababu; Homoni nyingi za kike (estrogen na progesterone) zikiwa katika kiwango kikubwa husababisha kuongezeka kwa mtiririko wa damu katika fizi, hii husababisha fizi kuwa sensitive na kuovereact kwa kitu chochote kinachoweza kuziirritate. Wanawake huwa ni sensitive kwa utando unaokua kwenye meno hasa wakati kiwango cha homoni zao kipo juu. Hali hiyo hupelekea fizi kuvimba na kuanza kutoa damu, hali hii isipotibiwa hupelekea ugonjwa kushika kasi na kuharibu mfupa unaoshikilia meno na kupeleka meno kulegea na kutoka. Homoni za mwili ni maisha ila magonjwa ya fizi yanaweza kuzuiwa na kutibiwa katika hatua za mwanzo kabisa. Nini hasa mwanamke anatakiwa kufanya? Anza kuzingatia na kuhakikis...

VIFAA VYA KULINDA KINYWA (MOUTHGUARDS)

MOUTH GUARDS                   Hebu fikiria kama ghafla umepoteza meno yako, tabasamu, kuongea na kula kutaathiriwa kwa kiwango kikubwa sana. Kujua jinsi ya kulinda meno na mdomo hasa wakati wa michezo ni jambo la muhimu sana. Mouthguards husaidia kulinda meno na midomo pale ambapo kuna nguvu inayoweza kupelekea ajali au kuumia kwa meno na midomo. Meno ya juu ya mbele yapo katika hatari kubwa sana ya kuumia kwa sababu yapo nje na yamesogea mbele kidogo ukilinganisha na meno ya chini. Wakati gani utumie Mouthguards? Linapofika suala la kulinda mdomo, mouthguards inatakiwa iwe kati ya vitu muhimu katika shughuli zote za michezo kuanzia mtu akiwa na umri mdogo. Kwa watoto ni muhimu sana kwa sababu michezo yao mingi huhusisha kugusana, kujigonga na kuanguka. Aina za Mouthguards Mouthguards hutengenezwa na madaktari wa meno baada ya kuchukua kipimo cha mdomo ambacho huitwa impression. Pia ku...

TATIZO LA KUSAGA MENO.

TATIZO LA KUSAGA MENO.   Asilimia kubwa ya watu wana tatizo la kusaga meno ambalo kitaalamu linafahamika kama "bruxism". Tatizo hili la kusaga meno huenda sambamba na kukaza kwa taya (jaw clenching) Kuna aina mbili la tatizo hili la kusaga meno au bruxism, sleep/noctunal bruxism ambalo hutokea wakati mtu akiwa amelala na diurnal/awake bruxism ambalo hutokea wakati mtu akiwa macho. Aina zote mbili zina vitu vinavyofanana ambavyo ni kusaga meno na kukaza kwa taya. Ni ngumu kugundua kama una tatizo la kusaga kwa sababu mara nyingi hutokea bila kufahamu lakini kama una hizi dalili basi una tatizo la kusaga meno  Maumivu ya taya na kupungua kwa kufunguka kwa mdomo Meno yaliyosagika na kuvunjika Maumivu ya kichwa Maumivu ya masikio Ingiwa mtu yoyote anaweza akapata tatizo hili ila huwapata sana watu wenye umri kuanzia miaka 20-40 Athari za kusaga meno. Kwanini watu wanasaga meno? Kuna sababu nyingi zinazopelekea watu kusaga meno, lakini inaaminika kuwa sa...

AFYA YA KINYWA NA MENO KWA WAJAWAZITO

AFYA YA KINYWA NA MENO KWA WAJAWAZITO Ujauzito ni kipindi ambacho mwanamke anakua ana mahitaji mengi na mabadiliko mengi katika mwili na baadhi ya mabadiliko hayo yana athari kwa afya ya kinywa na meno kama hakutakua na uangalizi mzuri wa kinywa na meno kwa kipindi cha ujauzito. Moja ya matatizo ya kinywa na meno yanayowapata wajawazito wengi ni tatizo la fizi kuvimba na kutoa damu ambayo kitaalamu inaitwa "pregnancy gingivitis au pregnancy tumour". Tatizo hili husababishwa na kuongezeka kwa kiwango cha homoni iitwayo "progesterone" ambayo huchangia kuongezeka kwa mtirirko wa damu kwenye fizi na kuzifanya ziwe sensitive, kuvimba na rahisi kutoa damu wakati wa kupiga mswaki. Mabadiliko ya kiwango cha homoni hii pia huwapa urahisi bakteria ambao husababisha magonjwa ya fizi kukua na kusababisha magonjwa ya fizi. Tatizo hili la fizi linaweza kutokea muda wowote kuanzia mwezi wa pili mpaka wa nane lakini huwa kwa kasi sana katika kipindi cha pili cha ujauzit...

UMRI NA AFYA YA KINYWA NA MENO

UMRI NA AFYA YA KINYWA NA MENO Umri ukiwa unaongezeka inakua ni muhimu zaidi kuwa muangalifu na afya ya kinywa na meno. Kuna imani potofu kuwa kadiri mtu anavyozeeka ndivyo anavyopoteza meno yake, SI KWELI.  Kama unapiga mswaki vizuri na kuwa muangalifu na afya ya kinywa na meno, meno yako yanaweza kubaki maisha yako yote. Kinywa hubadilika umri ukiwa unaongezeka, mishipa ya fahamu kwenye meno hubadilika na kuwa midogo zaidi na kukufanya kutohisi sana maumivu pale meno yanapotoboka. Kama utakua hufanyi check up ya meno mara kwa mara, hii hufanya matatizo yagundulike yakiwa katika hatua mbaya ambayo mara nyingine inaweza ikashindikana kutibiwa na kupeleke kupoteza meno. Kama unataka kujisikia vizuri, kuwa na fya na muonekano mzuri, utashangazwa na jinsi kinywa chenye afya kinaweza kukubadilisha. Vifuatavyo ni vidokezo vinavyoweza kukusaidia kudumisha na kuboresha afya ya kinywa na meno kwa maisha yako yote. Piga mswaki angalau mara mbili kwa siku kwa mswaki laini na d...

MATATIZO YA TUMBO NA AFYA YA MENO

MATATIZO YA TUMBO NA AFYA YA MENO Matatizo ya tumbo ya mara kwa mara yanawezaz kusababisha kulika kwa tabaka la juu kabisa la meno kwa mchakato ambao kitaalamu unaitwa "tooth erosion". Kulika kwa tabaka hilo la meno husababisha meno kuwa na muonekano mbaya na pia huhatarisha meno kutoboka. Matatizo ya Tumbo yanaathiri vipi Meno? Tumbo hutengeneza tindikali ya asili ambayo husaidia katika umen'genyaji wa chakula. Mara nyingine tindikali hiyo husafiri kwenye njia ya chakula mpaka mdomoni hasa baada ya kula chakula kingi. Kwa kawaida mate yetu huweka usawa wa tindikali hiyo na kila kitu huwa sawa. Lakini kwa wale ambao hupata tatizo la kubeua au kitaalamu huitwa " gastroesophageal reflux ". Hii husababisha tindikali kufika mdomoni mara nyingi sana, tindikali hii huanza kushambulia meno na kuondoa taratibu tabaka la juu kabisa la meno. Tatizo hili huwa linatokea sana wakati unapokua umelala kwa sababu mzunguko wa mate mdomoni huwa mdogo na hivyo kushind...

MATUMIZI YA ANTIBIOTICS KATIKA AFYA YA KINYWA NA MENO

 MATUMIZI YA ANTIBIOTICS KATIKA AFYA YA KINYWA NA MENO   Antibiotics hutolewa pale ambapo kuna maambukizi au ugonjwa unaosababishwa na bakteria. Linapofika suala la maumivu ya jino, antibiotics zinatakiwa kuepukwa isipokua pale ambapo kuna uhitaji sana wa kuzitumia. Kuwa na uelewa kuhusu antibiotics kutasaidia kuweza kuelezea vizuri jinsi ambavyo unajisikia kwa daktari wa meno na kupata jinsi ya kutatua tatizo. Kwa kujua dalili za maumivu ya jino daktari anaweza kujua ni matibabu gani yanafaa kulingana na tatizo. ni Daktari pekee ndiye anayejua ni wakati gani unafaa kutumia antibiotics na upi haufai kulingana na tatizo na maumivu. Antibiotics hutolewa mara nyingi kwa maambukizi au infection ambayo imesambaa na hii huweza kutambulika kama daktari akishakuona na kutambua ukubwa wa tatizo. Dawa ni za kipekee. Hatuwezi kushiriki kutumia mswaki mmoja si ndivyo? Basi ndivyo ilivyo kwenye madawa, dawa inayomsaidia mtu mmoja inaweza isifanye kazi kwa mtu mwingin...

DAWA YA KUSUKUTUA MDOMO

DAWA ZA KUSUKUTUA MDOMO Ingawa sio mbadala wa kupiga mswaki, matumizi ya dawa za kusukutua au mouthwash yanasaidia katika kuimarisha afya ya kinywa na meno. Kwanini tunahitaji kutumia Dawa za Kusukutua Mdomo? Kama ambavyo uzi wa kusafishia meno (dental floss) ufanyavyo, dawa za kusukutua mdomo pia hufika sehemu ambazo mswaki hauwezi kufika na husaidia kupunguza hatari ya kuoza meno na kupata magonjwa ya fizi na pia hufanya kinywa kiwe fresh na kuwa na harufu nzuri. Aina za Dawa za kusukutua Mdomo Dawa za kusukutua mdomo kwa ajili ya tiba (Therapeutic Mouthwash) ; Hizi ni dawa zenye viungo hai (active ingredients) kama flouride ambazo husaidia kuondoa utando juu ya meno, meno kuoza, magonjwa ya fizi na harufu mbaya ya kinywa. Na pia kuna ambazo ni maalumu kwa watu ambao wana matatizo ya kinywa kama vidonda au majeraha ya ajali.                                      ...

TATIZO LA KUKOSA PUMZI NA KUKOROMA WAKATI WA KULALA

TATIZO LA KUKOSA PUMZI  NA KUKOROMA WAKATI WA KULALA Kukosa pumzi wakati wa kulala (sleep apnea) ni tatizo ambalo hutokea wakati upumuaji wa kawaida huingiliwa wakati mtu akiwa usingizini. Kukoroma ni tatizo linalowapata watu wengi wanaopata shida ya ya kupumua wakati wakiwa usingizini ila sio wote wanaokoroma wanapata shida ya kupumua. Kuna aina mbili za kukosa pumzi wakati wa usingizi; Obstructive sleep apnea. Hii ndio ya kawaida na inawapata watu wengi. Hutokea pale njia ya hewa inapokua imezibwa wakati wa usingizi. Matatizo ya kiafya kama uzito uliopitiliza huchangia sana kwenye hili. Central sleep apnea. Hii hutokea pale ambapo ubongo unashindwa  kupeleka taarifa na kuamsha misuli ya upumuaji. Njia za hewa zinakua wazi ila ubongo hushindwa kuamsha misuli. Hii huwapata sana watu waliopooza, wenye saratani ya ubongo na moyo kushindwa kufanya kazi(heart failure). Tatizo la kukosa pumzi usingizini linaweza kumpata mtu yoyote katika umri wowote. Ingawa wan...

UNYONYAJI VIDOLE KWA WATOTO

UNYONYAJI WA VIDOLE KWA WATOTO   Unyonyaji wa vidole (hasa vidole gumba) kwa watoto ni jambo la kawaida na huwafanya watulie na kujisikia furaha na amani. Kunyonya vidole Gumba kuna athari gani kwa Meno? Kinywa cha mtoto hukua umri ukiwa unaongezeka na meno ya utu uzima yanapokua yanaanza kujitokeza kinywani. Unyonyaji wa vidole gumba huathiri  vitu vifutavyo;  ukuaji wa kinywa   mpangilio wa meno  ina uwezo wa kubadilisha muundo wa taya ya juu.                                                           Athari za unyonyaji wa vidole.  Ukubwa wa matatizo haya hutegemea na nguvu inayotumika kunyonya vidole. Kuna watoto ambao huegesha tu kidole kwenye midomo(lips) bila kukinyonya hawa athari zao huwa ndogo sana ukilinganisha na wale ambao hunyonya vidole vyao kwa nguvu na hua athari za...

NJIA ZA KUSAIDIA KUACHA UVUTAJI WA SIGARA NA MATUMIZI YA TUMBAKU

NJIA ZA KUSAIDIA KUACHA UVUTAJI WA SIGARA NA MATUMIZI YA TUMBAKU Tunafahamu kuwa uvutaji wa sigara na matumizi ya tumbaku ni hatari kwa afya, hivyo basi haitakua kitu kigeni kufahamu kuwa matumizi ya sigara na tumbaku yana athari kwa afya ya kinywa na meno pia. Matumizi ya sigara na tumbaku husababisha harufu mbaya ya kinywa, lakini huo ni mwanzo tu wa athari hizo. Matumizi ya sigara na tumbaku husababisha;  meno na ulimi kupata rangi nyeusi au "stains" vidonda vya midomoni kutopona kwa haraka hasa baada ya meno kutolewa Magonjwa ya fizi Saratani ya kinywa Kuacha matumizi ya sigara na tumbaku ni njia ya kupunguza athari za matumizi hayo. Ulevi au addiction ya nicotine ambayo inapatikana kwenye sigara inaweza kufanya ugumu wa kuacha matumizi ya sigara, hivyo basi hizi ni njia ambazo zinaweza kusaidia mtu kupunguza na mpaka kuacha kabisa matumizi ya sigara na tumbaku. Kuwa na lengo . Ukiamua kuacha matumizi ya sigara na tumbaku, weka lengo na weka tarehe am...

MADINI YA FLOURIDI

FAIDA ZA MADINI YA FLOURIDI (FLOURIDE) Flouridi ni madini ambayo kiasili hupatikana katika vyakula vingi na maji. Flouridi huungana na madini mengine katika meno na kutengeneza tabaka la enameli(tabaka la juu kabisa la meno) ambalo ni imara na sugu zaidi kwa tindikali ambayo husababisha meno kutoboka.    Tindikali hii katika meno huaribu tabaka la enameli kwa mchakato ambao kitaalamu huitwa "demineralization". Mchakato huu huanza kwa kudhoofisha tabaka la enameli na kupelekea kuanza kutengenezwa kwa mashimo madogo katika meno na inaweza kuendelea na kutengeneza mashimo makubwa zaidi na mwishoni hata kupoteza meno. Hatua za mwanzo za mchakato huu wa "demineralization" zinaweza kuzuiwa kwa kuweka madini ya flouride katika meno. Kuna njia mbili ambazo madini ya flouridi hulinda tabaka la enameli katika meno ambazo ni; Kimfumo Kwa njia ya kuweka moja kwa moja kwenye meno Kimfumo madini ya flouridi hufanya kazi wakati meno hutengenezwa na kukua kwa wa...

MDOMO MKAVU

MDOMO MKAVU (XEROSTOMIA) Mdomo mkavu au xerostomia ni hali ambayo husababisha uwepo wa kiwango kidogo cha mate mdomoni au kuzuia mate yasitengenezwe. Hali hii husababisha matatizo wakati wa kula, kumeza chakula, kuongea na pia ni chanzo kikubwa cha meno kuoza na harufu mbaya ya kinywa. Nini Husababisha Mdomo Kuwa Mkavu? Mdomo mkavu au xerostomia unaweza kusababishwa na baadhi ya madawa yanayotumika kutibu magonjwa fulani. Ukiwa na tatizo hili wakati unatumia dawa hizo, usiache kutumia bali hakikisha unampa taarifa daktari wako au daktari wa meno. Mdomo mkavu pia ni dalili ya magonjwa kama kisukari, hivyo basi ni vyema kutoa taarifa kwa daktari kuhusu tatizo hilo kama likiwa kwa muda mrefu. Dalili za Mdomo Mkavu Ukavu na mnato mdomoni Kupata shida wakati wa kula, kumeza na kuongea Ukavu wa midomo(lips) na kuwepo kwa vidonda kwenye midomo na koo Harufu mbaya ya kinywa Sababu hatarishi zinazopelekea kuwa na mdomo mkavu Athari za baadhi ya madawa Kisukari Ugonjwa...