
Kama umekua ukipata wasiwasi wa kwenda kumuona daktari wa meno, jua kwamba hauko peke yako. Pengine unahisi utapata maumivu au hujui nini daktari atafanya kulingana na atakachokiona.
Sababu za wasiwasi zinaweza kuwa; Kutokuwa na taarifa sahihi kutoka kwa daktari, kupata maumivu baada ya matibabu au mawazo hasi kuhusu matibabu ya meno.
Kwa sababu yoyote ile, timu nzuri ya madaktari itasaidia kuhakikisha afya yako ya kinywa na meno pamoja na kimawazo inakuwa nzuri. Unavyochelewa zaidi kumuona daktari wa meno ndivyo unavyokua kwenye hatari ya kupata matatizo makubwa zaidi na kusababisha matibabu yawe magumu zaidi. Mathalani, kumuona daktari wa meno mapema kutasaidia kufanya matibabu yawe rahisi na muda mfupi.
Zifuatazo ni njia ambazo unaweza kuzitumia ukiwa unaenda kumuona daktari wa meno ili kupunguza wasiwasi na kufanya uwe na tabasamu lenye uangavu.
- Ongea
-Mwambie daktari kuhusu wasiwasi wako
-Usiogope kuuliza maswali
-Kubaliana na lugha ya ishara kumwambia daktari kama kuna tatizo na usimshike kuingilia matibabu
-Ukihisi maumivu mwambie daktari
- Ondoa mawazo
- Vaa spika za masikioni na usikilize mziki
- Shika kitu mkononi na uwe unakichezea
- Fumba macho na ufikirie mambo yanayoleta furaha kama kuwa ufukweni au kwenye bustani nzuri
- Vuta pumzi
Hizi ndizo njia ambazo unaweza kuzitumia ili kuondoa wasiwasi wakati wa matibabu au kumuona daktari wa meno.
Kumbuka; DAKTARI WA MENO NI RAFIKI
Comments
Post a Comment