Skip to main content

DAWA YA KUSUKUTUA MDOMO

DAWA ZA KUSUKUTUA MDOMO


Image result for mouthwash
Ingawa sio mbadala wa kupiga mswaki, matumizi ya dawa za kusukutua au mouthwash yanasaidia katika kuimarisha afya ya kinywa na meno.

Kwanini tunahitaji kutumia Dawa za Kusukutua Mdomo?

Kama ambavyo uzi wa kusafishia meno (dental floss) ufanyavyo, dawa za kusukutua mdomo pia hufika sehemu ambazo mswaki hauwezi kufika na husaidia kupunguza hatari ya kuoza meno na kupata magonjwa ya fizi na pia hufanya kinywa kiwe fresh na kuwa na harufu nzuri.

Aina za Dawa za kusukutua Mdomo
  • Dawa za kusukutua mdomo kwa ajili ya tiba (Therapeutic Mouthwash); Hizi ni dawa zenye viungo hai (active ingredients) kama flouride ambazo husaidia kuondoa utando juu ya meno, meno kuoza, magonjwa ya fizi na harufu mbaya ya kinywa. Na pia kuna ambazo ni maalumu kwa watu ambao wana matatizo ya kinywa kama vidonda au majeraha ya ajali.
                                    Image result for therapeutic mouthwash
                                                         Mfano wa therapeutic mouthwash
  • Dawa za kusukutua ambazo sio za tiba (Cosmetic Mouthwash); Hizi husaidia kufanya kinywa kuwa na harufu na ladha nzuri lakini haisaidii katika kulinda meno dhidi ya kuoza au magonjwa ya fizi.
                                                       
                                               



                                                            Image result for cosmetic mouthwash
                                                         Mfano wa cosmetic mouthwash


Kuna baadhi ya dawa za kusukutua ambazo hutolewa kwa maandishi ya daktari (prescription) ila nyingi hupatikana kwenye maduka ya dawa. Ni vyema kuonana na daktari wa meno ili kupata ushauri zaidi wa aina gani ya dawa za kusukutua ambazo unafaa kutumia kulingana na mahitaji yako ya afya ya kinywa na meno.

Dawa za Kusukutua Mdomo kwa Watoto.
Dawa za kusukutua mdomo hazishauriwi kutumika kwa watoto chini ya miaka sita (6). Wanaweza kumeza dawa hizi kwa bahati mbaya na kusababisha kichefuchefu na hata kutapika.

NI VYEMA KUTAZAMA LEBO YA DAWA ZA KUSUKUTUA KABLA YA KUZITUMIA ILI KUJUA TAHADHARI ZA KUCHUKUA, MAELEKEZO YA MATUMIZI NA MAPENDEKEZO YA UMRI.

Comments

Popular posts from this blog

HOMONI NA AFYA YA KINYWA NA MENO - VITU AMBAVYO KILA MWANAMKE ANAPASWA KUJUA

 HOMONI ZA KIKE NA AFYA YA KINYWA NA MENO Uzito. Hisia, Mahitaji ya kimwili(sex drive). Afya ya kinywa na meno. Ni vitu ambavyo vinaweza kufanya afya yako ya mwili ikabadilika. Utashangazwa kujua jinsi mabadiliko ya homoni zako yanaweza kukufanya uwe katika hatari ya kupata magonjwa ya fizi. Sababu ni hii. Uwepo wa homoni nyingi za kike katika mwili wako unasababisha damu nyingi kutiririka katika fizi zako na kuzifanya ziwe sensitive na kuoverreact kwakitu chochote kitakachozikera(irritate). Wanawake wapo sensitive na uwepo wa uchafu katika meno yao pale ambapo homoni zao katika mwili zipo juu, hii  husababisha fizi kuvimba na kutoka damu na kama zisipotibiwa hupelekea kupoteza mfupa unaoshikilia meno na kupelekea meno kupotea. Homoni ni maisha na ni kitu kisichoepukika ila magonjwa ya fizi yanaweza kuzuiwa na kutibika katika hatua zake za mwanzo. Sasa nini kifanyike? Anza kwa kuwa makini na afya ya kinywa chako katika vipindi vitano katika maisha yako. 1. Balehe Mabadiliko ya...

PLASTIC FREE SMILES PROJECT 2023-2024

  Plastic Free Smiles project is an environmental and oral health project designed by Dr. Winfred Mgaya under the umbrella of Tanzania Oral Health Foundation. The project aims to raise awareness on the effects of plastic pollution to the environment specifically caused by plastic toothbrushes and advocating on the adoption of eco-friendly toothbrushes to reduce the plastic pollution caused by plastic toothbrushes. The project is structured to have two phases that will start from November 2023 to April 2024 and May 2024 to November 2024. The project includes physical meetings with target groups as well as online and social media campaigns OBJECTIVES The objective of the advocacy campaign is to raise awareness of the environmental impact of plastic toothbrushes while encouraging people to make the switch to eco-friendly toothbrushes. Specifically, the objectives are: 1. To educate the public on the harmful effects of plastic toothbrushes on the environment. 2. To promote t...

VINA SABA NA AFYA YA KINYWA NA MENO

       Je vinasaba vinaweza kutabari uwezekano wa kupata magonjwa ya fizi na meno kutoboka? Je, magonjwa ya kutoboka meno na fizi hurithishwa? Jibu kwa sasa ni HAPANA. Magonjwa ya meno kutoboka na fizi yanachangiwa sana na mazingira na mitindo ya maisha na sio vina saba au kurithishwa. Usafi wa kinywa, vitu unavyokula, matumizi ya tumbaku yana mchango mkubwa sana katika kupata magonjwa ya fizi na meno kutoboka. Vifaa vya uchunguzi vinavyotumiwa na daktari pamoja na picha za xray ndivyo husaidia kujua hali ya afya yako ya kinywa kwa sasa na kutabiri hali katika siku za mbeleni. Chukua hatua sasa katika kuzuia magonjwa ya fizi na meno kutoboka kwa kufanya yafuatayo Piga mswaki angalau mara mbili kwa siku Safisha sehemu ya katikati ya meno yako kwa kutumia uzi maalum au floss Kula chakula bora na chenye afya na punguza matumizi ya vyakula vyenye sukari Fanya uchunguzi wa afya ya kinywa angalau mara mbili kwa mwaka