MATATIZO YA TUMBO NA AFYA YA MENO
Matatizo ya tumbo ya mara kwa mara yanawezaz kusababisha kulika kwa tabaka la juu kabisa la meno kwa mchakato ambao kitaalamu unaitwa "tooth erosion". Kulika kwa tabaka hilo la meno husababisha meno kuwa na muonekano mbaya na pia huhatarisha meno kutoboka.
Matatizo ya Tumbo yanaathiri vipi Meno?
Tumbo hutengeneza tindikali ya asili ambayo husaidia katika umen'genyaji wa chakula. Mara nyingine tindikali hiyo husafiri kwenye njia ya chakula mpaka mdomoni hasa baada ya kula chakula kingi. Kwa kawaida mate yetu huweka usawa wa tindikali hiyo na kila kitu huwa sawa.
Lakini kwa wale ambao hupata tatizo la kubeua au kitaalamu huitwa "gastroesophageal reflux". Hii husababisha tindikali kufika mdomoni mara nyingi sana, tindikali hii huanza kushambulia meno na kuondoa taratibu tabaka la juu kabisa la meno. Tatizo hili huwa linatokea sana wakati unapokua umelala kwa sababu mzunguko wa mate mdomoni huwa mdogo na hivyo kushindwa kuondoa tindikali hiyo.
![]() |
| Meno yaliyomomonyoka kutokana na tindikali. |
Dalili za kuwa una tatizo la mmomonyoko wa tabaka la meno.
- Kupata hali ya ganzi au sensitivity ukiwa unakula vyakula au vinywaji vya baridi, moto au vyenye sukari.
- Meno kubadilika na kuwa ya njano
- Kama kuna meno yaliyozibwa, kubadilika rangi kwa sehemu zilizozibwa.
- Kupata meno kutoboka mara kwa mara
- Kupoteza meno
- Kutafuna bubble gum zisizo na sukari ili kuongeza utengenezwaji wa mate ambayo husaidia kutoa tindikali katika meno
- Kama una matatizo ya tumbo yanayopelekea kupata kiungulia au kubeua ni vizuri kumuona daktari ili kutibu chanzo cha tatizo hilo.
- Kuepuka matumizi ya pombe na sigara. Pombe na sigara huongeza kiwango cha tindikali katika kinywa na kufanya tatizo la kulika au kumomonyoka kwa meno liongezeke mara dufu.
- Kutokula masaa matatu kabla ya kulala kutasaidia kupunguza nafasi ya kubeua nakurudisha tindikali katika kinywa.
- Kumuona daktari wa meno ili kupata tiba mbadala na ushauri wa jinsi gani kuyatunza meno kulingana na tatizo ulilonalo.


Comments
Post a Comment