MOUTH GUARDS

Hebu fikiria kama ghafla umepoteza meno yako, tabasamu, kuongea na kula kutaathiriwa kwa kiwango kikubwa sana. Kujua jinsi ya kulinda meno na mdomo hasa wakati wa michezo ni jambo la muhimu sana.
Mouthguards husaidia kulinda meno na midomo pale ambapo kuna nguvu inayoweza kupelekea ajali au kuumia kwa meno na midomo. Meno ya juu ya mbele yapo katika hatari kubwa sana ya kuumia kwa sababu yapo nje na yamesogea mbele kidogo ukilinganisha na meno ya chini.
Wakati gani utumie Mouthguards?
Linapofika suala la kulinda mdomo, mouthguards inatakiwa iwe kati ya vitu muhimu katika shughuli zote za michezo kuanzia mtu akiwa na umri mdogo. Kwa watoto ni muhimu sana kwa sababu michezo yao mingi huhusisha kugusana, kujigonga na kuanguka.
Aina za Mouthguards
Mouthguards hutengenezwa na madaktari wa meno baada ya kuchukua kipimo cha mdomo ambacho huitwa impression. Pia kuna mouthguards ambazo huuzwa katika maduka ya dawa na vifaa vya michezo ambazo pia husaidia ingawa inaweza isiwe inatosha vizuri katika kinywa kwa sababu hazijaengenezwa maalumu kwa ajili ya kinywa kimoja.
Kuna mouthgards ambazo hutumika kwa watu ambao wanatatizo la kusaga meno wakati wa usiku, hizi huvaliwa tu ili kuzuia uharibifu wa meno pindi mtu anapokua anasaga meno.
MOUTHGUARDS NI MUHIMU KATIKA KUTUNZA NA KULINDA MENO DHIDI YA AJALI AMBAZO ZINAWEZA KUPELEKEA MENO KUUMIA. KAMA UNA MTOTO AU WEWE MWENYEWE UNASHIRIKI SANA KATIKA MICHEZO HAKIKISHA UNALINDA MENO YAKO KWA MOUTHGUARDS.
Comments
Post a Comment