Skip to main content

MAFUA NA KIKOHOZI; MAMBO MATANO UNAYOPASWA KUFANYA UKIWA NA MAFUA NA KIKOHOZI


        7 cold virus and flu myths and questions debunked | CBC News

Ukiwa na mafua na au kikohozi, kuweka mwili wako sawa na katika hali ya usafi ni jambo la msingi na muhimu na hii inahusisha usafi wa kinywa pia. Zifuatazo ni njia rahisi ambazo unaweza kuzitumia ili kuhakikisha afya ya kinywa na meno inabaki kuwa nzuri na imara wakati unaumwa.

  • Zingatia Usafi mzuri
Ukiwa unaumwa  mafua na kikohozi ni vyema kuziba mdomo na pua wakati wa kukohoa na kupiga chafya pia usisahau kuhakikisha afya ya kinywa chako inazingatiwa. Tafiti zinaonesha kwamba virusi vya mafua vina uwezo wa kukaa sehemu yenye unyevu kwa takribani masaa 72. Hivyo basi ni vyema kutoshirikiana kutumia mswaki mmoja kwa watu wawili pia ni vizuri kubadilisha mswaki mara baada ya kupona mafua ingawa asilimia za kupata mafua kutoka kwenye mswaki ni ndogo lakini ni vyema kuchukua tahadhari.
  • Tumia dawa ambazo hazina sukari
Kama inavyojulikana kwamba sukari ndio chanzo kikubwa cha meno kuoza, hivyo basi kutumia dawa ambazo zina sukari zinaweza kuleta athari kwenye meno na kusababisha kuoza. Inashauriwa kutumia dawa ambazo hazina sukari na kila ukinunua dawa hakikisha unasoma label na kujua kwamba haina sukari.
                       Covonia Chesty Sugar Free | Morrisons
  • Sukutua na kutema baada ya kutapika
Moja ya athari za mafua kwa baadhi ya watu ni kutapika. Unapotapika, tindikali iliyopo tumboni huja mdomoni na kusambaa kwenye meno. Ikikaa kwa muda inaweza ikasababisha kulika kwa meno hivyo basi inashauriwa kusukutua baada ya kutapika na kupiga mswaki nusu saa baada ya kutapika ili kuhakikisha tindikali yote imekwisha kwenye meno.
            Mouth Rinsing | e-DantSeva
  • Kunywa maji mengi kujikinga na ukavu wa mdomo
Ukiwa unaumwa unahitaji kunywa maji mengi kwa sababu nyingi ikiwemo kuzuia ukavu wa mdomo. Ukavu wa mdomo unachangia sana katika kusababisha meno kutoboka pia dawa za mafua nyingi husababisha kinywa kuwa kikavu hivyo basi inashauriwa kunywa maji mengi kuhakikisha mtiririko wa mate unabaki vizuri.
          15 benefits of drinking water and other water facts
  • Chagua vinywaji sahihi
Linapokuja suala la afya ya kinywa na mwili kwa ujumla, kinywaji kimoja huwa ndicho sahihi nacho ni MAJI. Ni vyema kuweka tabia ya kunywa maji ya kutosha kila siku. Vinywaji vingine sio mbaya kuvinywa lakini ni vyema kuhakikisha havina sukari. Wakati ambao unaumwa mafua na kikohozi muda mwingine unaweza kuwa unahitaji kitu cha moto ka ma chai, ni vyema kutotumia sukari nyingi na limao ambayo huwa ina madhara katika meno.



Comments

Popular posts from this blog

HOMONI NA AFYA YA KINYWA NA MENO - VITU AMBAVYO KILA MWANAMKE ANAPASWA KUJUA

 HOMONI ZA KIKE NA AFYA YA KINYWA NA MENO Uzito. Hisia, Mahitaji ya kimwili(sex drive). Afya ya kinywa na meno. Ni vitu ambavyo vinaweza kufanya afya yako ya mwili ikabadilika. Utashangazwa kujua jinsi mabadiliko ya homoni zako yanaweza kukufanya uwe katika hatari ya kupata magonjwa ya fizi. Sababu ni hii. Uwepo wa homoni nyingi za kike katika mwili wako unasababisha damu nyingi kutiririka katika fizi zako na kuzifanya ziwe sensitive na kuoverreact kwakitu chochote kitakachozikera(irritate). Wanawake wapo sensitive na uwepo wa uchafu katika meno yao pale ambapo homoni zao katika mwili zipo juu, hii  husababisha fizi kuvimba na kutoka damu na kama zisipotibiwa hupelekea kupoteza mfupa unaoshikilia meno na kupelekea meno kupotea. Homoni ni maisha na ni kitu kisichoepukika ila magonjwa ya fizi yanaweza kuzuiwa na kutibika katika hatua zake za mwanzo. Sasa nini kifanyike? Anza kwa kuwa makini na afya ya kinywa chako katika vipindi vitano katika maisha yako. 1. Balehe Mabadiliko ya...

UJUMBE SIKU YA AFYA YA KINYWA NA MENO DUNIANI 2025

 

PLASTIC FREE SMILES PROJECT 2023-2024

  Plastic Free Smiles project is an environmental and oral health project designed by Dr. Winfred Mgaya under the umbrella of Tanzania Oral Health Foundation. The project aims to raise awareness on the effects of plastic pollution to the environment specifically caused by plastic toothbrushes and advocating on the adoption of eco-friendly toothbrushes to reduce the plastic pollution caused by plastic toothbrushes. The project is structured to have two phases that will start from November 2023 to April 2024 and May 2024 to November 2024. The project includes physical meetings with target groups as well as online and social media campaigns OBJECTIVES The objective of the advocacy campaign is to raise awareness of the environmental impact of plastic toothbrushes while encouraging people to make the switch to eco-friendly toothbrushes. Specifically, the objectives are: 1. To educate the public on the harmful effects of plastic toothbrushes on the environment. 2. To promote t...