
Mate yana kazi kubwa na muhimu katika kuimarisha afya kinywa na meno. Hutokana na mfumo wa damu na hivyo huwa kama mkondo wa damu katika kinywa. Hii humaanisha kuwa kama ilivyo kwa damu, mate pia hufanya kazi kubwa katika kuimarisha na kulinda afya ya tishu laini na ngumu katika kinywa.
Mtiririko wa mate ukipungua katika kinywa, matatizo kama kuoza kwa meno na vidonda vya mdomoni huanza kujitokeza. Kutafuna ni njia mojawapo ambayo huamsha mtiririko wa mate katika kinywa, husababisha misuli kugandamiza tezi za mate ambazo huzalisha mate.
Kazi za mate ni pamoja na;
- Kuondoa mabaki ya vyakula yaliyoganda katika meno na fizi
- Kulainisha na kukivunja chakula ili kurahisisha kumeza
- Kusaidia kuimarisha ladha
- Kulinda dhidi ya maradhi yanayoweza kushambulia meno na tishu za kwenye kinywa
- Kufanya uso wa meno kuwa imara kwa kupakaza madini ya calcium, flouride na phosphate katika meno.
Ni muhimu kuhakikisha Kinywa kina Mate ya kutosha, kuepuka mdomo mkavu hakikisha unatafuna bubblegum ambazo hazina sukari ili kusaidia kuamsha tezi kuzalisha mate. Kama unahisi kuwa na mdomo mkavu kwa muda mrefu, hakikisha umeonana na daktari wa kinywa na meno ili kupata msaada zaidi.
Comments
Post a Comment