Skip to main content

KUTOBOA MIDOMO (ORAL PIERCINGS)

All About Oral Piercings - San Jose Dental Health Care | San Jose ...


Kutoboa mwili kumekua kitu maarufu siku za karibuni na imekua kama njia ya kujielezea na kujitambulisha. Kutoboa midomo kunaweza kuonekana ni kitu kizuri na cha kupendeza lakini kinaweza kuleta madhara makubwa kwa mwili na afya. Hii ni kwa sababu kinywa kina vijududu vingi sana ambavyo vinaweza kusababisha maambukizi na kuvimba hasa baada ya kutoboa sehemu za kinywa na midomo. 

Kama umetoboa ulimi, mashavu, midomo (lips) na kilimi (sehemu ya nyuma kabisa ya koo), hii inaathiri sana kuongea, kutafuna na pia kumeza, vilevile inaweza ikasababisha;
  • Maambukizi, maumivu na kuvimba. Kwa sababu ya uwingi wa bakteria katika kinywa, kutoboa sehemu za kinywa kunaweza sababisha maambukizi ambayo huwa pamoja na maumivu na kuvimba. Kuvimba kwa ulimi au sehemu aya nyuma ya koo kunaweza sababisha kukosa pumzi na hata kupoteza maisha.
  • Kuharibika kwa meno na fizi
  • Mzio au Allergy
  • Kuharibika kwa mishipa ya fahamu. Hii ni hasa kwa kutoboa ulimi. kunaweza kusababisha kuharibika kwa mishipa ya fahamu ya ulimi na hii hupelekea athari ya mlango wa fahamu wa ladha.
  • Kutokwa kwa mate mengi
  • Ugumu katika matibabu ya kinywa na meno hasa linapofika suala la mionzi wakati wa kuchukua picha za xray
  • Saratani ya kinywa 
Kama tayari umetoboa kinywa zingatia yafuatayo;
  • Muone daktariwa meno pindi tu unapoona dalili za maumivu, uvimbe sehemu uliyotoboa
  • Hakikisha unaiweka sehemu uliyotoboa safi kwa kusukutua na dawa ya kusukutua kila baada ya kula.
  • Angalia kama chuma kilichowekwa sehemu uliyotoboa kimekaza kuepuka kumeza 
  • Toa chuma wakati wa mazoezi
  • Muone daktari wa kinywa na meno mara kwa mara na hakikisha unasafisha kinywa mara mbili kwa siku
NJIA PEKEE YA KUEPUKA MATATIZO HAYA NI KUTOTOBOA KINYWA AU KUTOA VYUMA KABLA HAIJAKULETEA MATATIZO. KUTOBOA KINYWA HULETA MAJUKUMUA MAPYA KWENYE MAISHA KWA SABABU KUNAHITAJI UANGALIZI WA HALI YA JUU. USITOBOE KINYWA, ONGEA NA DAKTARI WA KINYWA NA MENO KWA USHAURI ZAIDI.

Comments

Popular posts from this blog

HOMONI NA AFYA YA KINYWA NA MENO - VITU AMBAVYO KILA MWANAMKE ANAPASWA KUJUA

 HOMONI ZA KIKE NA AFYA YA KINYWA NA MENO Uzito. Hisia, Mahitaji ya kimwili(sex drive). Afya ya kinywa na meno. Ni vitu ambavyo vinaweza kufanya afya yako ya mwili ikabadilika. Utashangazwa kujua jinsi mabadiliko ya homoni zako yanaweza kukufanya uwe katika hatari ya kupata magonjwa ya fizi. Sababu ni hii. Uwepo wa homoni nyingi za kike katika mwili wako unasababisha damu nyingi kutiririka katika fizi zako na kuzifanya ziwe sensitive na kuoverreact kwakitu chochote kitakachozikera(irritate). Wanawake wapo sensitive na uwepo wa uchafu katika meno yao pale ambapo homoni zao katika mwili zipo juu, hii  husababisha fizi kuvimba na kutoka damu na kama zisipotibiwa hupelekea kupoteza mfupa unaoshikilia meno na kupelekea meno kupotea. Homoni ni maisha na ni kitu kisichoepukika ila magonjwa ya fizi yanaweza kuzuiwa na kutibika katika hatua zake za mwanzo. Sasa nini kifanyike? Anza kwa kuwa makini na afya ya kinywa chako katika vipindi vitano katika maisha yako. 1. Balehe Mabadiliko ya...

UJUMBE SIKU YA AFYA YA KINYWA NA MENO DUNIANI 2025

 

PLASTIC FREE SMILES PROJECT 2023-2024

  Plastic Free Smiles project is an environmental and oral health project designed by Dr. Winfred Mgaya under the umbrella of Tanzania Oral Health Foundation. The project aims to raise awareness on the effects of plastic pollution to the environment specifically caused by plastic toothbrushes and advocating on the adoption of eco-friendly toothbrushes to reduce the plastic pollution caused by plastic toothbrushes. The project is structured to have two phases that will start from November 2023 to April 2024 and May 2024 to November 2024. The project includes physical meetings with target groups as well as online and social media campaigns OBJECTIVES The objective of the advocacy campaign is to raise awareness of the environmental impact of plastic toothbrushes while encouraging people to make the switch to eco-friendly toothbrushes. Specifically, the objectives are: 1. To educate the public on the harmful effects of plastic toothbrushes on the environment. 2. To promote t...