Skip to main content

MATUMIZI YA ANTIBIOTICS KATIKA AFYA YA KINYWA NA MENO

 MATUMIZI YA ANTIBIOTICS KATIKA AFYA YA KINYWA NA MENO 


Image result for antibiotics

Antibiotics hutolewa pale ambapo kuna maambukizi au ugonjwa unaosababishwa na bakteria. Linapofika suala la maumivu ya jino, antibiotics zinatakiwa kuepukwa isipokua pale ambapo kuna uhitaji sana wa kuzitumia.
Kuwa na uelewa kuhusu antibiotics kutasaidia kuweza kuelezea vizuri jinsi ambavyo unajisikia kwa daktari wa meno na kupata jinsi ya kutatua tatizo. Kwa kujua dalili za maumivu ya jino daktari anaweza kujua ni matibabu gani yanafaa kulingana na tatizo. ni Daktari pekee ndiye anayejua ni wakati gani unafaa kutumia antibiotics na upi haufai kulingana na tatizo na maumivu.
Antibiotics hutolewa mara nyingi kwa maambukizi au infection ambayo imesambaa na hii huweza kutambulika kama daktari akishakuona na kutambua ukubwa wa tatizo.

Dawa ni za kipekee.

Hatuwezi kushiriki kutumia mswaki mmoja si ndivyo? Basi ndivyo ilivyo kwenye madawa, dawa inayomsaidia mtu mmoja inaweza isifanye kazi kwa mtu mwingine. Dawa zinazosaidia kutibu mafua au ugonjwa mwingine zinaweza zisisaidie kutibu matatizo ya meno na muda mwingine kupelekea kupata athari. Daktari wa meno anajua ni dawa ipi itakayokufaa kwa tatizo lako.

Athari za Kutumia Antibiotics mara kwa mara:

Matumizi yaliyopitiliza ya antibiotics husababisha ugumu katika kutibu maambukizi yanayosababishwa na bakteria (antibiotic resistant bacteria). Tumia antibiotics pale tu unapoandikiwa na daktari, hii itasaidia kufanya dawa ziwe na nguvu pale zinapotumika.


SIO KILA MAUMIVU YA JINO YANATIBIWA NA ANTIBIOTICS. USITUMIE ANTIBIOTICS BILA USHAURI NA MAELEKEZO YA DAKTARI, UKIWA NA MAUMIVU YA JINO NI VYEMA KUMUONA DAKTARI WA MENO KWA AJILI YA MATIBABU SAHIHI.

Comments

Popular posts from this blog

HOMONI NA AFYA YA KINYWA NA MENO - VITU AMBAVYO KILA MWANAMKE ANAPASWA KUJUA

 HOMONI ZA KIKE NA AFYA YA KINYWA NA MENO Uzito. Hisia, Mahitaji ya kimwili(sex drive). Afya ya kinywa na meno. Ni vitu ambavyo vinaweza kufanya afya yako ya mwili ikabadilika. Utashangazwa kujua jinsi mabadiliko ya homoni zako yanaweza kukufanya uwe katika hatari ya kupata magonjwa ya fizi. Sababu ni hii. Uwepo wa homoni nyingi za kike katika mwili wako unasababisha damu nyingi kutiririka katika fizi zako na kuzifanya ziwe sensitive na kuoverreact kwakitu chochote kitakachozikera(irritate). Wanawake wapo sensitive na uwepo wa uchafu katika meno yao pale ambapo homoni zao katika mwili zipo juu, hii  husababisha fizi kuvimba na kutoka damu na kama zisipotibiwa hupelekea kupoteza mfupa unaoshikilia meno na kupelekea meno kupotea. Homoni ni maisha na ni kitu kisichoepukika ila magonjwa ya fizi yanaweza kuzuiwa na kutibika katika hatua zake za mwanzo. Sasa nini kifanyike? Anza kwa kuwa makini na afya ya kinywa chako katika vipindi vitano katika maisha yako. 1. Balehe Mabadiliko ya...

UJUMBE SIKU YA AFYA YA KINYWA NA MENO DUNIANI 2025

 

PLASTIC FREE SMILES PROJECT 2023-2024

  Plastic Free Smiles project is an environmental and oral health project designed by Dr. Winfred Mgaya under the umbrella of Tanzania Oral Health Foundation. The project aims to raise awareness on the effects of plastic pollution to the environment specifically caused by plastic toothbrushes and advocating on the adoption of eco-friendly toothbrushes to reduce the plastic pollution caused by plastic toothbrushes. The project is structured to have two phases that will start from November 2023 to April 2024 and May 2024 to November 2024. The project includes physical meetings with target groups as well as online and social media campaigns OBJECTIVES The objective of the advocacy campaign is to raise awareness of the environmental impact of plastic toothbrushes while encouraging people to make the switch to eco-friendly toothbrushes. Specifically, the objectives are: 1. To educate the public on the harmful effects of plastic toothbrushes on the environment. 2. To promote t...