
Uzito, mhemko (mood) na afya ya kinywa na meno. Kuna kitu kimoja ambacho kinaendesha hivi vitu vyote, nacho ni homoni.
Unaweza ukajiuliza ni vipi homoni zinauhusiano na afya ya kinywa na meno kwa mwanamke, hii ndio sababu; Homoni nyingi za kike (estrogen na progesterone) zikiwa katika kiwango kikubwa husababisha kuongezeka kwa mtiririko wa damu katika fizi, hii husababisha fizi kuwa sensitive na kuovereact kwa kitu chochote kinachoweza kuziirritate. Wanawake huwa ni sensitive kwa utando unaokua kwenye meno hasa wakati kiwango cha homoni zao kipo juu. Hali hiyo hupelekea fizi kuvimba na kuanza kutoa damu, hali hii isipotibiwa hupelekea ugonjwa kushika kasi na kuharibu mfupa unaoshikilia meno na kupeleka meno kulegea na kutoka.
Homoni za mwili ni maisha ila magonjwa ya fizi yanaweza kuzuiwa na kutibiwa katika hatua za mwanzo kabisa. Nini hasa mwanamke anatakiwa kufanya? Anza kuzingatia na kuhakikisha afya ya kinywa na meno inakua nzuri katika vipindi hivi vitano vya maisha.
Kipindi Cha Balehe
Kipindi hiki huwa kuna mabadiliko ya homoni ambayo huweza kupelekea msichana kuanza kupata uvimbe, wekundu na kuvuja damu kwenye fizi. Tiba mbadala ni kuhakisha unapiga mswaki mara mbili kwa siku kwa kutumia dawa ya meno yenye madini ya flouride kuhakikisha hakuna utando unabaki kwenye meno.
Kipindi Cha Hedhi.

Mara nyingi huwa kuna mabadiliko ya hali ya kinywa siku chache kabla ya hedhi na wakati wahedhi ikiendelea. Mabadiliko hayo ni pamoja na fizi kuvimba, kuvuja damu na kutokea kwa vidonda mdomoni. Yote hayo husababishwa na mabadiliko ya homoni. Hali hii huisha punde tu hedhi inapokwisha, ila tunashauri sana kufanya usafi wa kinywa mara dufu katika kipindi hiki ili kuzuia magonjwa ya fizi. na kwasababu hedhi ni kila mwezi, inaweza kufanya tatizo la fizi likawa kubwa zaidi.
Kipindi cha Matumizi ya dawa za kuzuia Mimba.

Moja ya athari za matumizi ya dawa za kuzuia mimba ni kuvimba na kuvuja damu kwa fizi. Ingawa dawa za sasa wamepunguza kiwango cha homoni hizi ila ni muhimu kujua athari zake kwa afya ya kinywa na meno. Tunashauri kwa anayetumia hizi dawa afanye uchunguzi wa kinywa mara kwa mara na pia usafi wa kinywa uzingatiwe.
Kipindi Cha Ujauzito.

Kipindi cha ujauzito ni kipindi ambacho wanawake wengi hupata matatizo ya meno na fizi. Moja ya hali inayotokea kipindi hiki ni kuvimba kwa fizi. Tunashauri, kwa kina mama wote wajawazito, kuhakikisha wanafanya usafi wa kinywa mara dufu na pia kufanya uchunguzi na usafi wa kinywa kwa daktari wa meno mara kwa mara.
Kipindi cha kuisha kwa vipindi vya hedhi (menopause)

Menopause ni mabadiliko makubwa sana kwa maisha ya mwanamke. Kipindi hiki mwanamke huwa anapata mabadiliko katika ladha ya ulimi, kukauka kwa mdomo, ganzi na zaidi ya yote ni kupoteza sehemu za mifupa. Hii yote husababishwa na mabadiliko ya homoni. Ukavu wa mdomo husababisha mzunguko wa mate kupungua mdomoni na hii hupelekea kuwepo kwa nafasi ya meno kutoboka kwa urahisi. Unachokula kinaweza kufanya mabadiliko hasa inapofika suala la mdomo mkavu. Epuka kula vitu vyenye sukari, chumvi na pilipili kwa wingi. Epuka pombe, sigara na vinywaji vyenye caffein hivi hufanya hali ya mdomo mkavu izidi kuwa mbaya zaidi.
MABADILIKO YA HOMONI KWENYE MWILI YANA ATHARI KUBWA KWA AFYA YA KINYWA NA MENO KWA MWANAMKE. ZINGATIA KILA KIPINDI CHA MAISHA NA CHUKUA HATUA STAHIKI KUHAKIKISHA AFYA YA KINYWA NA MENO INAKUA NZURI NA IMARA
Comments
Post a Comment