
Kama una jino lililoharibika sana, kuoza au lenye maambukizi (infection), daktari wa meno anaweza akashauri matibabu ya kusafisha mizizi au root canal. Matibabu ya kusafisha mizizi ya jino yanatumika kuokoa jino pale inapohitajika badala ya kulitoa.
Nini Hufanyika katika matibabu ya kusafisha mizizi ya jino?
| Jinsi jino lilivyo kwa muonekano wa ndani. |
Jino huwa na nafasi ndani yake ambayo huwa na mishipa ya fahamu na damu ambayo hulifanya jino liwe hai. Sehemu hii inaweza kupata maambukizi kama;
- Una tundu kwenye jino ambalo ni kubwa sana
- Matibabu ya muda mrefu ambayo yanaweza kusababisha matatizo kwa sehemu hii.
- Jino likivunjika au kupasuka
- Ajali yoyote kwenye jino
Nini ha kutegemea wakati wa matibabu haya?
Matibabu ya kusafisha mizizi huweza kuchukua awamu mbili mpaka tatu ili kumalizika. Huwa ni matibabu ambayo hayana maumivu kwa sababu daktari hutumia ganzi wakati wa matibabu na mwisho wa matibabu maumivu uliyokuwa nayo mwanzoni yanatakiwa kuwa yamekwisha kabisa.
Kabla ya matibabu daktari atafanya yafuatayo;
- Atapiga picha ya x ray ili kuangalia jino na mfupa unaolizunguka
- Atakuweka ganzi ili kuondoa maumivu na kukufanya uwe mtulivu na vizuri wakati wa matibabu
- Atatengeneza uwazi juu ya jino ili kuifikia sehemu yenye mishipa ya damu na fahamu.
- Atatoa mishipa ya damu na fahamu na damu kutoka kwenye jino na sehemu ya mizizi ambayo hufahamika kama mifereji au canals
- Atasafisha mifereji ya mizizi kwa kutumia dawa ambazo husaidia kuondoa vijidudu vilivyopo humo.
- Mwisho wa matibabu mifereji ya mizizi huzibwa ili kuzuia kitu chochote kisiingie kwenye jino, na pia jino huzibwa tayari kwa kuendelea na matumizi yake. Kama jino limeharibika sana wakati mwingine linaweza kuhitaji kuwekewa kofia au crow ni vizn ambayo huifanya jino liwe imara zaidi.
Jino lililozibwa baada ya Matibabu ya kusafisha mizizi hukaa kwa muda gani?
Likiwa linasafishwa vizuri jino hukaa kwa maisha yote. Muhimu ni kusafisha meno vizuri kwa dawa yenye madini ya flouride, kusafisha katikati ya meno kwa uzi maalumu au floss, na pia kumuona daktari wa meno mara kwa mara ili kuhakikisha meno yanabaki kuwa na afya na imara.
Comments
Post a Comment