Skip to main content

MFUNGO NA AFYA YA KINYWA NA MENO


       Muslim Fasting Month Of Ramadan To Start Thursday – Independent ...

Watu wengi wanatokea kusahau kufanya usafi wa kinywa na meno wakiamini kuwa hakuna tatizo litawapata katika kipindi cha mfungo. Kuhakikisha usafi wa kinywa na meno utasaidia kupunguza harufu mbaya ya kinywa na kinywa kuwa kikavu.

NINI HUTOKEA UKIWA UMEFUNGA?

Kufunga husababisha kuongezeka kwa kampaundi za madini ya sulphur katika kinywa na husababisha harufu mbaya ya kinywa. Watu wengi wanaamini kuwa kufunga husaidia kutibu magonjwa ya fizi, hii sio kweli. Kuongezeka kwa kampaundi za madini ya sulphur huenda sambamba na kupungua kwa mtiririko wa mate katika kinywa ambayo husababisha kutengenezwa kwa matabaka ya uchafu katika meno kitu ambacho moja kwa moja hupelekea matatizo ya fizi na meno kutoboka.

JINSI YA KUTUNZA AFYA YA KINYWA NA MENO KIPINDI CHA MFUNGO.

Changamoto nyingi za afya ya kinywa na meno huwepo kipindi cha mfungo. Wengi wamezoea harufu mbaya ya kinywa katika kipindi cha mfungo na huwa wanahisi ni jambo la kawaida. Fanya mambo yafuatayo ili kuimarisha afya yako ya kinywa na meno;


  • Sukutua mdomo kuzuia harufu mbaya ya kinywa. Ingawa inakatazwa kumeza chochote kipindi cha masaa ya mfungo, ila unaweza kusukutua mdomo na kuhakikisha unatema kila kitu bila kumeza. Hii husaidia kuondoa ukavu wa mdomo na kuzuia meno kutoboka. Baada ya msaa ya mfungo hakikisha unakunywa maji au juisi za matunda. Epuka vinywaji vyenye caffein na chumvi kwa kuwa husababisha ukavu wa mdomo.
          Why you should never rinse your mouth with water after brushing
  • Safisha meno kwa dawa ya meno yenye flouride kila baada ya masaa ya mfungo. Hii husaidia kuondoa tabaka la vyakula ambalo huwa na bakteria wanaosababisha meno kutoboka.
          Why Falling Asleep Without Brushing Your Teeth Is Actually Pretty ...
  • Fanya uangalizi wa kinywa mara kwa mara. Inashauriwa kufanya uangalizi wa kinywa kabla ya mfungo haujaanza na mara baada ya mfungo kuisha ili kuhakikisha kama kuna tatizo lolote basi linatatuliwa. Pia kama kuna huduma yoyote inayohitaji dharura basi ni vizuri ukamwona daktari wa meno ili kufanya huduma ya haraka.
              Dentist
  • Lishe bora. Lishe bora ni muhimu kwa afya ya mwili. Vyakula vyenye sukari husababisha meno kuoza. Hivyo basi unapokua unafuturu hakikisha unakula chakula bora chenye virutubisho muhimu kwani kukosa virutubisho kuna madhara mengi kwa afya ya kinywa. Kunywa vimiminika vingi hasa maji na kula matunda ili kuimarisha afya ya kinywa.
              Importance of Balanced Diet - How It Can Enhance Your Health
  • Punguza ulaji wa Vyakula vinavyonata. Baada ya masaa ya mfungo, watu wengi hupenda kula vyakula vyenye kunata na sukari nyingi kama tende, chocolate na kadhalika. Vyakula hivi hunasa kwenye meno na huwa ni ngumu kuvitoa. hiyo husababisha meno kuoza na matatizo mengi ya kinywa. Hivyo basi unashauriwa kupunguza ulaji wa vyakula hivi ili kupunguza uuwezekano wa meno kuoza.
                                                  Food to Avoid with Braces | Orthodontics Exclusively
Mfungo ni kipindi muhimu sana katika maisha yetu, ingawa huwa tunatokea kusahau vitu vidogo kama afya ya kinywa na meno. Afya mbaya ya kinywa huleta madhara kwa mwili mzima, matatizo ya meno huleta shida wakati wa kula. Kusukutua, kupiga mswaki na kula chakula au lishe bora husaidia kuimarisha afya ya kinywa na meno. Kumbuka kumuona daktari wa meno kabla haujaanza mfungo na baada ya mfungo kuisha ili kuhakikisha afya ya kinywa na meno ipo imara. Muone daktari kila uhisipo maumivu na wakati wa dharura.

Comments

Popular posts from this blog

HOMONI NA AFYA YA KINYWA NA MENO - VITU AMBAVYO KILA MWANAMKE ANAPASWA KUJUA

 HOMONI ZA KIKE NA AFYA YA KINYWA NA MENO Uzito. Hisia, Mahitaji ya kimwili(sex drive). Afya ya kinywa na meno. Ni vitu ambavyo vinaweza kufanya afya yako ya mwili ikabadilika. Utashangazwa kujua jinsi mabadiliko ya homoni zako yanaweza kukufanya uwe katika hatari ya kupata magonjwa ya fizi. Sababu ni hii. Uwepo wa homoni nyingi za kike katika mwili wako unasababisha damu nyingi kutiririka katika fizi zako na kuzifanya ziwe sensitive na kuoverreact kwakitu chochote kitakachozikera(irritate). Wanawake wapo sensitive na uwepo wa uchafu katika meno yao pale ambapo homoni zao katika mwili zipo juu, hii  husababisha fizi kuvimba na kutoka damu na kama zisipotibiwa hupelekea kupoteza mfupa unaoshikilia meno na kupelekea meno kupotea. Homoni ni maisha na ni kitu kisichoepukika ila magonjwa ya fizi yanaweza kuzuiwa na kutibika katika hatua zake za mwanzo. Sasa nini kifanyike? Anza kwa kuwa makini na afya ya kinywa chako katika vipindi vitano katika maisha yako. 1. Balehe Mabadiliko ya...

UJUMBE SIKU YA AFYA YA KINYWA NA MENO DUNIANI 2025

 

PLASTIC FREE SMILES PROJECT 2023-2024

  Plastic Free Smiles project is an environmental and oral health project designed by Dr. Winfred Mgaya under the umbrella of Tanzania Oral Health Foundation. The project aims to raise awareness on the effects of plastic pollution to the environment specifically caused by plastic toothbrushes and advocating on the adoption of eco-friendly toothbrushes to reduce the plastic pollution caused by plastic toothbrushes. The project is structured to have two phases that will start from November 2023 to April 2024 and May 2024 to November 2024. The project includes physical meetings with target groups as well as online and social media campaigns OBJECTIVES The objective of the advocacy campaign is to raise awareness of the environmental impact of plastic toothbrushes while encouraging people to make the switch to eco-friendly toothbrushes. Specifically, the objectives are: 1. To educate the public on the harmful effects of plastic toothbrushes on the environment. 2. To promote t...