Skip to main content

UKWELI KUHUSU NJIA ZA ASILI ZINAZOTUMIKA KUNG'ARISHA MENO

Linapofika suala la kufanya meno yawe meupe, kuna njia nyingi ambazo zimekua zikiwekwa kwenye mitandao ya jamii na hata magazeti. Watu wengi wakiulizwa ni njia gani wanahisi wataweza kuifanya tabasamu lao liwe zuri zaidi majibu yao ni kwa kufanya meno yawe meupe zaidi.

Tabasamu lenye afya huja katika njia tofauti, ingawa inatamanisha kufikiri kwamba vitu tulivyonavyo jikoni vinaweza vikawa ufumbuzi wa tabasamu zuri. Njia kuwa ya asili haimaanishi ni njia ya kiafya. Njia za kiasili zinaweza kusababisha matatizo makubwa kuliko faida ambayo unaiwaza kuipata. Zifuatazo ni baadhi ya njia ambazo watu huhisi ni sahihi lakini kiafya zina madhara katika meno yako.

MAGADI (BAKING SODA)
Watu hutumia mchanganyo wa magadi na tindikali zitokanazo na matunda kama machungwa na mananasi.
                       Lemon and baking soda
Ukweli ni kwamba, kula matunda kiafya ni vizuri lakini mchanganyo wa magadi na juice za matunda ambao unatumika kufanya meno yawe meupe una madhara makubwa kwenye meno. Husababisha meno kulika na kuyafanya yawe sensitive na kupata ganzi muda mwingi.

              
MKAA

Mkaa hutumika peke yake na pia ukiwa na mchanganyo wa magadi au dawa ya kusukutua iitwayo hydrogen peroxide
                             Activated charcoal

Hakuna uthibitisho wowote kuwa mkaa au dawa za meno zenye mkaa zinafanya meno yawe meupe zaidi. Badala yake mkaa huleta athari ileile ya magadi kwa kufanya meno kulika na kuacha tabaka la meno ambalo ni sensitive kuwa nje na hii hupelekea hata meno kuonekana njano zaidi.

BADO UNAHITAJI MENO YAKO YAWE MEUPE???

                Patient getting her teeth whitened at the dentist
Njia nzuri na pekee zinazofanya meno kuwa meupe ni tabia za kila siku za usafi wa kinywa  ambazo ni;
  • Kupiga mswaki mara mbili kwa siku kila baada ya kula
  • Kutumia dawa za meno ambazo zinawea kufanya meno kuwa meupe ambazo zimethibitishwa na madaktari wa meno
  • Punguza matumizi ya vyakula na vinywaji ambavyo vinaacha rangi kwenye meno
  • Usivute sigara
  • Fanya usafi wa kinywa kitaalamu na kumuona daktari wa meno mara mbili kwa mwaka
Kama unahitaji kufanya meno meupe kwa utaratibu tofauti ni vyema ukaongea na daktari wa meno na kujua njia ipi itakufaa zaidi. Kuna njia tofauti zinazotumika kitaalamu kufanya meno yawe meupe, z nyumbani na ambazo hufanywa na daktari wa meno katika kliniki. Hakikisha njia unayotumia ni salama

Comments

Popular posts from this blog

HOMONI NA AFYA YA KINYWA NA MENO - VITU AMBAVYO KILA MWANAMKE ANAPASWA KUJUA

 HOMONI ZA KIKE NA AFYA YA KINYWA NA MENO Uzito. Hisia, Mahitaji ya kimwili(sex drive). Afya ya kinywa na meno. Ni vitu ambavyo vinaweza kufanya afya yako ya mwili ikabadilika. Utashangazwa kujua jinsi mabadiliko ya homoni zako yanaweza kukufanya uwe katika hatari ya kupata magonjwa ya fizi. Sababu ni hii. Uwepo wa homoni nyingi za kike katika mwili wako unasababisha damu nyingi kutiririka katika fizi zako na kuzifanya ziwe sensitive na kuoverreact kwakitu chochote kitakachozikera(irritate). Wanawake wapo sensitive na uwepo wa uchafu katika meno yao pale ambapo homoni zao katika mwili zipo juu, hii  husababisha fizi kuvimba na kutoka damu na kama zisipotibiwa hupelekea kupoteza mfupa unaoshikilia meno na kupelekea meno kupotea. Homoni ni maisha na ni kitu kisichoepukika ila magonjwa ya fizi yanaweza kuzuiwa na kutibika katika hatua zake za mwanzo. Sasa nini kifanyike? Anza kwa kuwa makini na afya ya kinywa chako katika vipindi vitano katika maisha yako. 1. Balehe Mabadiliko ya...

VINA SABA NA AFYA YA KINYWA NA MENO

       Je vinasaba vinaweza kutabari uwezekano wa kupata magonjwa ya fizi na meno kutoboka? Je, magonjwa ya kutoboka meno na fizi hurithishwa? Jibu kwa sasa ni HAPANA. Magonjwa ya meno kutoboka na fizi yanachangiwa sana na mazingira na mitindo ya maisha na sio vina saba au kurithishwa. Usafi wa kinywa, vitu unavyokula, matumizi ya tumbaku yana mchango mkubwa sana katika kupata magonjwa ya fizi na meno kutoboka. Vifaa vya uchunguzi vinavyotumiwa na daktari pamoja na picha za xray ndivyo husaidia kujua hali ya afya yako ya kinywa kwa sasa na kutabiri hali katika siku za mbeleni. Chukua hatua sasa katika kuzuia magonjwa ya fizi na meno kutoboka kwa kufanya yafuatayo Piga mswaki angalau mara mbili kwa siku Safisha sehemu ya katikati ya meno yako kwa kutumia uzi maalum au floss Kula chakula bora na chenye afya na punguza matumizi ya vyakula vyenye sukari Fanya uchunguzi wa afya ya kinywa angalau mara mbili kwa mwaka

UJUMBE SIKU YA AFYA YA KINYWA NA MENO DUNIANI 2025