UNYONYAJI WA VIDOLE KWA WATOTO
Unyonyaji wa vidole (hasa vidole gumba) kwa watoto ni jambo la kawaida na huwafanya watulie na kujisikia furaha na amani.
Kunyonya vidole Gumba kuna athari gani kwa Meno?
Kinywa cha mtoto hukua umri ukiwa unaongezeka na meno ya utu uzima yanapokua yanaanza kujitokeza kinywani. Unyonyaji wa vidole gumba huathiri vitu vifutavyo;
- ukuaji wa kinywa
- mpangilio wa meno
- ina uwezo wa kubadilisha muundo wa taya ya juu.
| Athari za unyonyaji wa vidole. |
Ni Muda gani watoto huacha kunyonya vidole?
Katika umri wa miaka miwili mpaka minne watoto wengi huacha kunyonya vidole. Kama ukiona kuna mabadiliko katika mpangilio wa meno ya watoto na pia kama mtoto anaendelea kunyonya vidole hata baada ya umri huo kufika basi ni vyema kumuona daktari wa kinywa na meno.
Nawezaje kumsaidia mtoto kuacha kunyonya vidole?
- Watoto wengi hunyonya vidole anapokua anahisi hana amani na anahitaji faraja. Zingatia sana katika kumfanya mtoto asiwe na wasiwasi na kumfariji muda mwingi
- Msifie pale anapokua hanyonyi kidole
- Onana na daktari wa meno. Daktari wa meno atasaidia kushauri ni njia gani nzuri ya kuzuia mtoto kunyonya vidole na pia kuongea na mtoto kuhusu athari za kunyonya vidole
UNYONYAJI WA VIDOLE KWA WATOTO NI JAMBO LA KAWAIDA KUTOKEA LAKINI LIKIFANYIKA KWA MUDA MREFU LINA ATHARI KWA MENO YAO.
Comments
Post a Comment