Skip to main content

NJIA ZA KUSAIDIA KUACHA UVUTAJI WA SIGARA NA MATUMIZI YA TUMBAKU

NJIA ZA KUSAIDIA KUACHA UVUTAJI WA SIGARA NA MATUMIZI YA TUMBAKU


Image result for quitting smoking

Tunafahamu kuwa uvutaji wa sigara na matumizi ya tumbaku ni hatari kwa afya, hivyo basi haitakua kitu kigeni kufahamu kuwa matumizi ya sigara na tumbaku yana athari kwa afya ya kinywa na meno pia. Matumizi ya sigara na tumbaku husababisha harufu mbaya ya kinywa, lakini huo ni mwanzo tu wa athari hizo. Matumizi ya sigara na tumbaku husababisha;
  •  meno na ulimi kupata rangi nyeusi au "stains"
  • vidonda vya midomoni kutopona kwa haraka hasa baada ya meno kutolewa
  • Magonjwa ya fizi
  • Saratani ya kinywa
Kuacha matumizi ya sigara na tumbaku ni njia ya kupunguza athari za matumizi hayo. Ulevi au addiction ya nicotine ambayo inapatikana kwenye sigara inaweza kufanya ugumu wa kuacha matumizi ya sigara, hivyo basi hizi ni njia ambazo zinaweza kusaidia mtu kupunguza na mpaka kuacha kabisa matumizi ya sigara na tumbaku.
  1. Kuwa na lengo. Ukiamua kuacha matumizi ya sigara na tumbaku, weka lengo na weka tarehe ambayo utaanza taratibu za kuacha matumizi ya sigara na tumbaku na onana na daktari wa meno kwa ushauri na msaada katika mchakato huo.
  2. Usifanye peke yako. Ni rahisi kuacha matumizi ya sigara na tumbaku kama ukipata msaada kutoka kwa marafiki na familia. Omba msaada wao na uwaambie wapi wanaweza kusaidia, tumia muda mwingi na watu wanaopenda ufanikiwe katika lengo lako na zungumza na watu walioweza kuacha matumizi ya sigara na tumbaku wakupe ushauri na uzoefu wao katika mchakato huo.
  3. Usikae bila kazi. Weka mbadala wa tabia ya uvutaji wa sigara kwa kufanya mazoezi na mambo mengine ambayo hayahusishi marafiki na watumiaji wa sigara pia tumia bubble gums zisizo na sukari kuuweka mdogo busy hii inasaidia pia kupunguza meno kutoboka.
  4. Epuka vitu vinavyopelekea utumie sigarana tumbaku. Epuka marafiki wanaotumia sigara, matumizi ya pombe, kahawa, msongo wa mawazo, tupa vitu vinavyotumika wakati wa kuvuta sigara, tembele sehemu ambazo uvutaji wa sigara hauruhusiwi.
  5. Jipongeze. Kuacha matumizi ya sigara na tumbaku sio kitu rahisi, kila saa, siku wiki ambayo inapita bila matumizi ya sigara au tumbaku inahitaji pongezi. Kwa kila pesa unayoitunza kwa kutotumia sigara unaweza jipongeza kwa kula vizuri.
MATUMIZI YA SIGARA NA TUMBAKU NI HATARI KWA AFYA YA KINYWA NA MENO NA AFYA YA MWILI KWA UJUMLA. KUACHA MATUMIZI HAYO KUTASAIDIA KUPUNGUZA ATHARI HIZO.  
KUACHA MATUMIZI YA SIGARA NA TUMBAKU INAWEZEKANA, WEKA LENGO NA ANZA SASA.

Comments

Popular posts from this blog

HOMONI NA AFYA YA KINYWA NA MENO - VITU AMBAVYO KILA MWANAMKE ANAPASWA KUJUA

 HOMONI ZA KIKE NA AFYA YA KINYWA NA MENO Uzito. Hisia, Mahitaji ya kimwili(sex drive). Afya ya kinywa na meno. Ni vitu ambavyo vinaweza kufanya afya yako ya mwili ikabadilika. Utashangazwa kujua jinsi mabadiliko ya homoni zako yanaweza kukufanya uwe katika hatari ya kupata magonjwa ya fizi. Sababu ni hii. Uwepo wa homoni nyingi za kike katika mwili wako unasababisha damu nyingi kutiririka katika fizi zako na kuzifanya ziwe sensitive na kuoverreact kwakitu chochote kitakachozikera(irritate). Wanawake wapo sensitive na uwepo wa uchafu katika meno yao pale ambapo homoni zao katika mwili zipo juu, hii  husababisha fizi kuvimba na kutoka damu na kama zisipotibiwa hupelekea kupoteza mfupa unaoshikilia meno na kupelekea meno kupotea. Homoni ni maisha na ni kitu kisichoepukika ila magonjwa ya fizi yanaweza kuzuiwa na kutibika katika hatua zake za mwanzo. Sasa nini kifanyike? Anza kwa kuwa makini na afya ya kinywa chako katika vipindi vitano katika maisha yako. 1. Balehe Mabadiliko ya...

UJUMBE SIKU YA AFYA YA KINYWA NA MENO DUNIANI 2025

 

PLASTIC FREE SMILES PROJECT 2023-2024

  Plastic Free Smiles project is an environmental and oral health project designed by Dr. Winfred Mgaya under the umbrella of Tanzania Oral Health Foundation. The project aims to raise awareness on the effects of plastic pollution to the environment specifically caused by plastic toothbrushes and advocating on the adoption of eco-friendly toothbrushes to reduce the plastic pollution caused by plastic toothbrushes. The project is structured to have two phases that will start from November 2023 to April 2024 and May 2024 to November 2024. The project includes physical meetings with target groups as well as online and social media campaigns OBJECTIVES The objective of the advocacy campaign is to raise awareness of the environmental impact of plastic toothbrushes while encouraging people to make the switch to eco-friendly toothbrushes. Specifically, the objectives are: 1. To educate the public on the harmful effects of plastic toothbrushes on the environment. 2. To promote t...