TATIZO LA KUSAGA MENO.

Asilimia kubwa ya watu wana tatizo la kusaga meno ambalo kitaalamu linafahamika kama "bruxism". Tatizo hili la kusaga meno huenda sambamba na kukaza kwa taya (jaw clenching)
Kuna aina mbili la tatizo hili la kusaga meno au bruxism, sleep/noctunal bruxism ambalo hutokea wakati mtu akiwa amelala na diurnal/awake bruxism ambalo hutokea wakati mtu akiwa macho. Aina zote mbili zina vitu vinavyofanana ambavyo ni kusaga meno na kukaza kwa taya.
Ni ngumu kugundua kama una tatizo la kusaga kwa sababu mara nyingi hutokea bila kufahamu lakini kama una hizi dalili basi una tatizo la kusaga meno
- Maumivu ya taya na kupungua kwa kufunguka kwa mdomo
- Meno yaliyosagika na kuvunjika
- Maumivu ya kichwa
- Maumivu ya masikio
| Athari za kusaga meno. |
Kwanini watu wanasaga meno?
Kuna sababu nyingi zinazopelekea watu kusaga meno, lakini inaaminika kuwa sababu kubwa ni msongo wa mawazo na wasiwasi. Na hii ndio sababu hasa tatizo hili huwapata sana vijana. Tatizo la kukosa pumzi na matumizi ya madawa ya kulevya pia ni sababu kubwa ya tatizo la kusaga meno.
Unawezaje kuzuia kusaga meno?
Hakuna tiba maalumu ya kuzuia kusaga meno, ila kuna njia kadhaa za kupunguza kusaga meno na athari zake.
- Kuvaa mouthguards ambazo husaidia kupunguza kusagika kwa meno
- Kupata tiba ya kisaikolojia kupunguza msongo wa mawazo na wasiwasi
- Kumuona Daktari wa meno kama una dalili mojawapo ya zilizotajwa hapo juu
![]() |
| Mouthguard, kifaa cha kupunguza athari za kusaga meno |

Comments
Post a Comment