UMRI NA AFYA YA KINYWA NA MENO
Umri ukiwa unaongezeka inakua ni muhimu zaidi kuwa muangalifu na afya ya kinywa na meno. Kuna imani potofu kuwa kadiri mtu anavyozeeka ndivyo anavyopoteza meno yake, SI KWELI. Kama unapiga mswaki vizuri na kuwa muangalifu na afya ya kinywa na meno, meno yako yanaweza kubaki maisha yako yote.
Kinywa hubadilika umri ukiwa unaongezeka, mishipa ya fahamu kwenye meno hubadilika na kuwa midogo zaidi na kukufanya kutohisi sana maumivu pale meno yanapotoboka. Kama utakua hufanyi check up ya meno mara kwa mara, hii hufanya matatizo yagundulike yakiwa katika hatua mbaya ambayo mara nyingine inaweza ikashindikana kutibiwa na kupeleke kupoteza meno.
Kama unataka kujisikia vizuri, kuwa na fya na muonekano mzuri, utashangazwa na jinsi kinywa chenye afya kinaweza kukubadilisha. Vifuatavyo ni vidokezo vinavyoweza kukusaidia kudumisha na kuboresha afya ya kinywa na meno kwa maisha yako yote.
- Piga mswaki angalau mara mbili kwa siku kwa mswaki laini na dawa ya meno yenye madini ya flouridi.
- Safisha meno katika nafasi ya jino na jino kwa kutumia floss angalau mara moja kwa siku.
- Kama unatumia meno bandia, hakikisha unasafisha meno hayo na kuvua angalau kwa msaa nane kwa siku.
- Kunywa maji yenye madini ya flouridi mara kwa mara
- Kama unatumia sigara basi fanya mipango ya kupunguza na kuacha kabisa
- Muone daktari wa meno mara kwa mara angalau mara mbili kwa mwaka (kila baada ya miezi sita)

Comments
Post a Comment