MDOMO MKAVU (XEROSTOMIA)

Mdomo mkavu au xerostomia ni hali ambayo husababisha uwepo wa kiwango kidogo cha mate mdomoni au kuzuia mate yasitengenezwe. Hali hii husababisha matatizo wakati wa kula, kumeza chakula, kuongea na pia ni chanzo kikubwa cha meno kuoza na harufu mbaya ya kinywa.
Nini Husababisha Mdomo Kuwa Mkavu?
- Mdomo mkavu au xerostomia unaweza kusababishwa na baadhi ya madawa yanayotumika kutibu magonjwa fulani. Ukiwa na tatizo hili wakati unatumia dawa hizo, usiache kutumia bali hakikisha unampa taarifa daktari wako au daktari wa meno.
- Mdomo mkavu pia ni dalili ya magonjwa kama kisukari, hivyo basi ni vyema kutoa taarifa kwa daktari kuhusu tatizo hilo kama likiwa kwa muda mrefu.
- Ukavu na mnato mdomoni
- Kupata shida wakati wa kula, kumeza na kuongea
- Ukavu wa midomo(lips) na kuwepo kwa vidonda kwenye midomo na koo
- Harufu mbaya ya kinywa
- Athari za baadhi ya madawa
- Kisukari
- Ugonjwa unaosababisha kuwa na majimaji machache mwilini ambao pia huathiri uwepo wa machozi katika macho Sjögren's syndrome
- Ukosefu wa kinga mwilini UKIMWI
- Msongo wa mawazo
- Presha ya damu isiyodhibitiwa
- Magonjwa ya tezi za mate
- Saratani na matibabu yake hasa ya mionzi
- Kunywa maji ya vuguvugu kwa wingi
- Epuka kunywa maji ya moto au baridi sana
- Kunywa vinywaji visivyo na sukari na epuka vinywaji vyenye kaboni
- Epuka vinywaji vyenye caffein, caffein husababisha ukavu mdomoni.
- Hakikisha unakunywa maji kila unapokula chakula
- Tumia bubble gum zisizo na sukari kusaidia utengenezaji wa mate
- Tumia dawa za kusukutua zisizokua na alcohol
Comments
Post a Comment