USAFI WA ULIMI
Tofauti na meno, ulimi una uso ambao sio laini na hutengeneza mazingira mazuri kwa vijidudu (bakteria) kuishi na kustawi au kuzaliana. Ulimi huwa na vijidudu wengi ukilinganisha na meno na hii husababisha harufu mbaya ya kinywa. Kama huna matatizo ya meno au fizi basi bakeria waliopo kwenye ulimi ndio sababu kubwa ya harufu mbaya ya kinywa.
Jinsi Ya Kusafisha Ulimi
Ukiwa umesafisha meno yako kwa usahihi, umakini wa usafi unatakiwa uelekezwe kwenye ulimi.Kusafisha ulimi husaidia kuondoa bakteria katika maeneo yote ya ulimi. Sehemu ya mbele ya ulimi huwa safi mara nyingi lakini sehemu ya nyuma ni muhimu kusafishwa. Kuna vifaa maalumu vya kusafishia ulimi ambavyo huitwa "tongue cleaner"
vimetengenezwa madhubuti kwa ajilin hiyo lakini vikikosekana, mswaki
unaweza ukasaidia. Ukiwa unasafisha ulimi, anza kwa kuweka kiasi kidogo cha dawa ya meno kwenye mswaki na uanze kusafisha ulimi kwa kuanzia nyuma kwenda mbele ukitumia presha ndogo na kama ukianza kusikia maumivu basi unashauriwa kumaliza kusafisha.
| Jinsi ya kusafisha Ulimi. |
| Kifaa maalumu cha kusafishia ulimi "Tongue Cleaner" |
Ulimi unatakiwa usafishwe kila unapopiga mswaki. Kama kinywa kinakua kikavu na kuwa na harufu pia unashauriwa kusafisha ulimi.
Comments
Post a Comment