SARATANI YA KINYWA
Saratani ni ukuaji wa seli za mwili usiodhibitiwa ambao hupelekea kuvamia tishu za jirani na kuziharibu.
Saratani ya kinywa hutokea kama kidonda au ukuaji wa tishu usiopotea. Saratani ya kinywa hujumuisha saratani ya midomo (lips), ulimi, mashavu, chini ya ulimi, taya ya juu, na koo. saratani ya kinywa inaweza kuhatarisha maisha isipogundulika na kutibiwa mapema.
DALILI ZA SARATANI YA KINYWA.
- Uvimbe kwenye maeneo mbalimbali ya kinywa
- Kutokwa na damu katika kinywa kusikokua na sababu
- Kupata ganzi, kutohisi chochote katika kinywa na maumivu wakati wa kugusa eneo lolote la kinywa, uso au shingo
- Uwepo wa vidonda kwenye kinywa uso au shingo ambavyo huvuja damu kwa urahisi na kutopona kwa wiki mbili au zaidi.
- Maumivu ya sikio
- Kutoweza kula, kuongea na kuchezesha taya au ulimi
- Kupungua uzito kwa ghafla
Ukiwa na dalili hizi tafadhali onana na Daktari wa kinywa na meno Haraka
NANI YUPO KATIKA HATARI YA KUPATA SARATANI YA KINYWA?
Kwa mujibu wa shirika la Saratani Marekani, wanaume wako katika hatari mara mbili zaidi kuliko wanawake na wanaume wenye umri wa miaka 50 au zaidi wapo kwenye hatari zaidi.
Sababu hatarishi zinazopelekea kupata saratani ya kinywa;
- Uvutaji wa sigara
- Ulaji wa ugoro. Hii husababisha hasa saratani ya midomo(lips) na mashavu.
- Unywaji wa pombe kupindukia
- Kuwepo na historia ya saratani katika familia
- Uwepo wa kirusi cha Human Papilloma Virus.
- Usivute sigara au kutumia ugoro
- Hakikisha unakula mlo kamili
- Fanya maangalizi ya afya ya kinywa na meno mara kwa mara ili kugundua tatizo mapema likiwepo. Asilimia 25% ya saratani huwakuta watu ambao sio watumiaji wa tumbaku au pombe.
Comments
Post a Comment