HOMONI ZA KIKE NA AFYA YA KINYWA NA MENO
Uzito. Hisia, Mahitaji ya kimwili(sex drive). Afya ya kinywa na meno. Ni vitu ambavyo vinaweza kufanya afya yako ya mwili ikabadilika.
Utashangazwa kujua jinsi mabadiliko ya homoni zako yanaweza kukufanya uwe katika hatari ya kupata magonjwa ya fizi. Sababu ni hii. Uwepo wa homoni nyingi za kike katika mwili wako unasababisha damu nyingi kutiririka katika fizi zako na kuzifanya ziwe sensitive na kuoverreact kwakitu chochote kitakachozikera(irritate). Wanawake wapo sensitive na uwepo wa uchafu katika meno yao pale ambapo homoni zao katika mwili zipo juu, hii husababisha fizi kuvimba na kutoka damu na kama zisipotibiwa hupelekea kupoteza mfupa unaoshikilia meno na kupelekea meno kupotea.
Homoni ni maisha na ni kitu kisichoepukika ila magonjwa ya fizi yanaweza kuzuiwa na kutibika katika hatua zake za mwanzo. Sasa nini kifanyike? Anza kwa kuwa makini na afya ya kinywa chako katika vipindi vitano katika maisha yako.
1. Balehe
Mabadiliko ya homoni katika kipindi hiki yanaweza kupelekea magonjwa ya fizi na kuwaacha wasichana wengi kupata vidonda, damu kutoka na uvimbe katika fizi. unahitaji kufanya usafi wa kinywa mara mbili kwa siku kwa kutumia dawa yenye madini ya flouride, kusafisha meno kwa kutumia uzi maalum au floss na kumuona daktari wa kinywa na meno mara kwa mara.
2. Hedhi
Unaweza usihisi mabadiliko yoyote katika kinywa chako siku chache kabla ya hedhi, lakini kama ikitokea kupata vidonda mdomoni, fizi kuvimba na kutoa damu basi sababu kubwa huwa ni mabadiliko ya kiwango cha homoni na huisha pale tu siku za hedhi zinapokwisha. ikitokea dalili hizo zinaendelea basi kuna sababu nyingine zaidi ya homoni, ni vizuri kumuona daktari wa kinywa na meno kwa msaada zaidi.
3. Matumizi ya vidonge vya uzazi wa mpango
Matatizo ya fizi ni moja ya athari za matumizi ya vidonge vya uzazi wa mpango ambayo wanawake wengi wamekua wakikumbana nayo. Habari njema ni kwamba sasa dawa nyingi zimepunguzwa homoni na kupelekea kupunguza athari ya matatizo ya fizi kwa kiwango kikubwa. Ni vyema kumjulisha daktari wako wa kinywa na meno kama unatumia dawa za uzazi wa mpango kwa sababu;
- Kuna baadhi ya dawa ambazo zinaweza kufanya nguvu ya vidonge vya uzazi wa mpango kupungua hivyo basi ni vyema daktari akafahamu ili kuziepuka
- Ukitolewa jino unakuwa kwenye hatari ya kupata maumivu zaidi kwa tafiti zinavyoonesha, hivyo ni vyema daktari akafahamu ili kuzuia athari hiyo mapema.
Comments
Post a Comment