Skip to main content

MAJIPU KATIKA KINYWA

MAJIPU KATIKA KINYWA (DENTAL ABSCESS)
Image result for dental abscess
Majipu katika kinywa (dental abscess) ni uvimbe ambao unakua na majimaji ya njano au usaha. Majipu katika kinywa yapo ya aina mbili; majipu yapatikanayo kwenye fizi (periodontal abscess) na majipu yapatikanayo kwenye meno (periapical abcess).

Nini husababisha Majipu katika kinywa?

Majipu hutengenezwa pale ambapo vijidudu au bakteria waliopo mdomoni wanapata mazingira mazuri ya kusababisha maambukizi (infection). Majipu hutengeneza kizuizi sehemu ambayo bakteria wamesababisha maambukizi na kuzuia yasisambae sehemu nyingine ya mwili.

Majipu ya fizi hutokea pale bakteria wanapotengeneza maambukizi kati ya fizi na meno, na hii ni matokeo ya mabaki ya vyakula kukwama sehemu hizo. Majipu ya fizi hutumia muda kujitengeneza na mara nyingi hutokea kwa watu wenye magonjwa ya fizi ya muda mrefu.
Image result for periodontal abscess


Majipu ya meno hutokea kwenye ncha ya mzizi wa jino na hutokea pale mishipa fahamu inapoelekea kufa au imekufa kabisa.


Image result for dental abscess
Jipu katika Meno

Dalili za Majipu katika Kinywa
  • Maumivu yenye kupwita
  • Uvimbe katika maeneo ya kinywa wenye usaha
  • Fizi kuwa nyekundu na kuuma
  • Maumivu ya jino wakati wa kula au kukiwa na msukumo katika jino
  • Harufu mbaya katika kinywa
  • Taste mbaya katika kinywa
Ni muhimu kutozipuuza dalili za majipu katika kinywa. Majipu ya kinywa yanaweza kukaa kwa muda mrefu kama yasipopatiwa matibabu sahihi.  Majipu yasipotibiwa yanaweza kusababisha madhara kwa meno yenyewe, mfupa unaozunguka meno, misuli ya shingo, kifua na kufika mbali hata kwenye mzunguko wa damu ambako kunaweza kusababisha matatizo makubwa zaidi.

Jinsi ya kuzuia majipu katika kinywa.

Majipu katika kinywa yanaweza kuzuiwa kwa kuhakikisha unafanya usafi wa kinywa kila siku na kwa usahihi, kuhakikisha hakuna mabaki ya chakula yanabaki katika meno na zaidi checkup za mara kwa mara kwa Daktari wa Meno.


Comments

Popular posts from this blog

HOMONI NA AFYA YA KINYWA NA MENO - VITU AMBAVYO KILA MWANAMKE ANAPASWA KUJUA

 HOMONI ZA KIKE NA AFYA YA KINYWA NA MENO Uzito. Hisia, Mahitaji ya kimwili(sex drive). Afya ya kinywa na meno. Ni vitu ambavyo vinaweza kufanya afya yako ya mwili ikabadilika. Utashangazwa kujua jinsi mabadiliko ya homoni zako yanaweza kukufanya uwe katika hatari ya kupata magonjwa ya fizi. Sababu ni hii. Uwepo wa homoni nyingi za kike katika mwili wako unasababisha damu nyingi kutiririka katika fizi zako na kuzifanya ziwe sensitive na kuoverreact kwakitu chochote kitakachozikera(irritate). Wanawake wapo sensitive na uwepo wa uchafu katika meno yao pale ambapo homoni zao katika mwili zipo juu, hii  husababisha fizi kuvimba na kutoka damu na kama zisipotibiwa hupelekea kupoteza mfupa unaoshikilia meno na kupelekea meno kupotea. Homoni ni maisha na ni kitu kisichoepukika ila magonjwa ya fizi yanaweza kuzuiwa na kutibika katika hatua zake za mwanzo. Sasa nini kifanyike? Anza kwa kuwa makini na afya ya kinywa chako katika vipindi vitano katika maisha yako. 1. Balehe Mabadiliko ya...

UJUMBE SIKU YA AFYA YA KINYWA NA MENO DUNIANI 2025

 

PLASTIC FREE SMILES PROJECT 2023-2024

  Plastic Free Smiles project is an environmental and oral health project designed by Dr. Winfred Mgaya under the umbrella of Tanzania Oral Health Foundation. The project aims to raise awareness on the effects of plastic pollution to the environment specifically caused by plastic toothbrushes and advocating on the adoption of eco-friendly toothbrushes to reduce the plastic pollution caused by plastic toothbrushes. The project is structured to have two phases that will start from November 2023 to April 2024 and May 2024 to November 2024. The project includes physical meetings with target groups as well as online and social media campaigns OBJECTIVES The objective of the advocacy campaign is to raise awareness of the environmental impact of plastic toothbrushes while encouraging people to make the switch to eco-friendly toothbrushes. Specifically, the objectives are: 1. To educate the public on the harmful effects of plastic toothbrushes on the environment. 2. To promote t...