HARUFU MBAYA YA KINYWA
NINI HUSABABISHA HARUFU MBAYA YA KINYWA?
Unaweza ukahisi kwamba harufu mbaya ya kinywa husababishwa hasa na vyakula kama vitunguu na vitunguu saumu, lakini unaweza kustaajabu kwa kufahamu kwamba vijududu (bakteria) waliopo katika ulimi ndio chanzo kikubwa cha harufu mbaya ya kinywa. Tafiti zinaonesha kwamba takataka zitolewazo na bakteria hawa ambazo zina uwepo wa kampaundi ya sulphur ndio sababu kubwa ya harufu mbaya ya kinywa. Mbali na chakula harufu mbaya ya kinywa inaweza kusababishwa na usafi mdogo wa kinywa, utumiaji wa tumbaku na baadhi ya magonjwa.
SABABU ZA KUWA NA HARUFU MBAYA YA KINYWA.
- Vyakula; vyakula kama vitunguu ni sababu kubwa ya harufu mbaya ya kinywa lakini pia vyakula vinavyonasa na kubaki kwenye meno au kati ya jino na jino husababisha mkusanyiko wa bakteria na kuleta harufu mbaya
- Usafi mdogo wa kinywa; kutosafisha kinywa husababisha uwepo wa utando katika meno, fizi na ulimi ambao kitaalamu huitwa plaque, utando huu huwa na bakteria ambao husababisha harufu mbaya ya kinywa.
- Matumizi ya tumbaku; Tumbaku huleta harufu mbaya ya kinywa ambayo ni ya muda mrefu na hii hutokana na nicotine ambayo ipo kwenye tumbaku na pia upungufu wa mtiririko wa mate katika kinywa.
- Magonjwa; magonjwa ya mfumo wa hewa na chakula ni chanzo kimojawapo cha harufu mbaya ya kinywa. Ni muhimu kufanya uchunguzi wa afya kama harufu mbaya ya kinywa ni ya muda mrefu.
Kuondokana na harufu mbaya ya kinywa unatakiwa kupiga mswaki kwa usahihi angalau mara mbili kwa siku kila baada ya kula, kusafisha katikati ya meno "flossing" kwa kutumia uzi maalumu "Floss"
Kudumisha harufu nzuri ya kinywa wakati ambao hupigi mswaki fanya yafuatayo;
- Sukutua na maji safi kila baada ya kula
- Sukutua kwa dawa ya kusukutua kinywa
- Tafuna bubblegum ambazo hazina sukari ili kuongeza mtirirko wa mate katika kinywa
- Kula matunda na carrots ambazo husaidia kuondoa mabaki ya chakula katika kinywa
- Kula kiafya, upungufu wa vitamins huweza kusababisha harufu mbaya ya kinywa
HAKIKISHA UNASAFISHA KINYWA KILA SIKU KWA USAHIHI NA KWA KUTUMIA DAWA YA MENO SAHIHI, DAWA YA KUSUKUTUA NA UZI WA KUSAFISHIA MENO.

Comments
Post a Comment