Skip to main content

Posts

Showing posts from February, 2020

UNYONYAJI VIDOLE KWA WATOTO

UNYONYAJI WA VIDOLE KWA WATOTO   Unyonyaji wa vidole (hasa vidole gumba) kwa watoto ni jambo la kawaida na huwafanya watulie na kujisikia furaha na amani. Kunyonya vidole Gumba kuna athari gani kwa Meno? Kinywa cha mtoto hukua umri ukiwa unaongezeka na meno ya utu uzima yanapokua yanaanza kujitokeza kinywani. Unyonyaji wa vidole gumba huathiri  vitu vifutavyo;  ukuaji wa kinywa   mpangilio wa meno  ina uwezo wa kubadilisha muundo wa taya ya juu.                                                           Athari za unyonyaji wa vidole.  Ukubwa wa matatizo haya hutegemea na nguvu inayotumika kunyonya vidole. Kuna watoto ambao huegesha tu kidole kwenye midomo(lips) bila kukinyonya hawa athari zao huwa ndogo sana ukilinganisha na wale ambao hunyonya vidole vyao kwa nguvu na hua athari za...

NJIA ZA KUSAIDIA KUACHA UVUTAJI WA SIGARA NA MATUMIZI YA TUMBAKU

NJIA ZA KUSAIDIA KUACHA UVUTAJI WA SIGARA NA MATUMIZI YA TUMBAKU Tunafahamu kuwa uvutaji wa sigara na matumizi ya tumbaku ni hatari kwa afya, hivyo basi haitakua kitu kigeni kufahamu kuwa matumizi ya sigara na tumbaku yana athari kwa afya ya kinywa na meno pia. Matumizi ya sigara na tumbaku husababisha harufu mbaya ya kinywa, lakini huo ni mwanzo tu wa athari hizo. Matumizi ya sigara na tumbaku husababisha;  meno na ulimi kupata rangi nyeusi au "stains" vidonda vya midomoni kutopona kwa haraka hasa baada ya meno kutolewa Magonjwa ya fizi Saratani ya kinywa Kuacha matumizi ya sigara na tumbaku ni njia ya kupunguza athari za matumizi hayo. Ulevi au addiction ya nicotine ambayo inapatikana kwenye sigara inaweza kufanya ugumu wa kuacha matumizi ya sigara, hivyo basi hizi ni njia ambazo zinaweza kusaidia mtu kupunguza na mpaka kuacha kabisa matumizi ya sigara na tumbaku. Kuwa na lengo . Ukiamua kuacha matumizi ya sigara na tumbaku, weka lengo na weka tarehe am...

MADINI YA FLOURIDI

FAIDA ZA MADINI YA FLOURIDI (FLOURIDE) Flouridi ni madini ambayo kiasili hupatikana katika vyakula vingi na maji. Flouridi huungana na madini mengine katika meno na kutengeneza tabaka la enameli(tabaka la juu kabisa la meno) ambalo ni imara na sugu zaidi kwa tindikali ambayo husababisha meno kutoboka.    Tindikali hii katika meno huaribu tabaka la enameli kwa mchakato ambao kitaalamu huitwa "demineralization". Mchakato huu huanza kwa kudhoofisha tabaka la enameli na kupelekea kuanza kutengenezwa kwa mashimo madogo katika meno na inaweza kuendelea na kutengeneza mashimo makubwa zaidi na mwishoni hata kupoteza meno. Hatua za mwanzo za mchakato huu wa "demineralization" zinaweza kuzuiwa kwa kuweka madini ya flouride katika meno. Kuna njia mbili ambazo madini ya flouridi hulinda tabaka la enameli katika meno ambazo ni; Kimfumo Kwa njia ya kuweka moja kwa moja kwenye meno Kimfumo madini ya flouridi hufanya kazi wakati meno hutengenezwa na kukua kwa wa...

MDOMO MKAVU

MDOMO MKAVU (XEROSTOMIA) Mdomo mkavu au xerostomia ni hali ambayo husababisha uwepo wa kiwango kidogo cha mate mdomoni au kuzuia mate yasitengenezwe. Hali hii husababisha matatizo wakati wa kula, kumeza chakula, kuongea na pia ni chanzo kikubwa cha meno kuoza na harufu mbaya ya kinywa. Nini Husababisha Mdomo Kuwa Mkavu? Mdomo mkavu au xerostomia unaweza kusababishwa na baadhi ya madawa yanayotumika kutibu magonjwa fulani. Ukiwa na tatizo hili wakati unatumia dawa hizo, usiache kutumia bali hakikisha unampa taarifa daktari wako au daktari wa meno. Mdomo mkavu pia ni dalili ya magonjwa kama kisukari, hivyo basi ni vyema kutoa taarifa kwa daktari kuhusu tatizo hilo kama likiwa kwa muda mrefu. Dalili za Mdomo Mkavu Ukavu na mnato mdomoni Kupata shida wakati wa kula, kumeza na kuongea Ukavu wa midomo(lips) na kuwepo kwa vidonda kwenye midomo na koo Harufu mbaya ya kinywa Sababu hatarishi zinazopelekea kuwa na mdomo mkavu Athari za baadhi ya madawa Kisukari Ugonjwa...

MAJIPU KATIKA KINYWA

MAJIPU KATIKA KINYWA (DENTAL ABSCESS) Majipu katika kinywa ( dental abscess ) ni uvimbe ambao unakua na majimaji ya njano au usaha. Majipu katika kinywa yapo ya aina mbili; majipu yapatikanayo kwenye fizi ( periodontal abscess ) na majipu yapatikanayo kwenye meno (periapical abcess). Nini husababisha Majipu katika kinywa? Majipu hutengenezwa pale ambapo vijidudu au bakteria waliopo mdomoni wanapata mazingira mazuri ya kusababisha maambukizi ( infection ). Majipu hutengeneza kizuizi sehemu ambayo bakteria wamesababisha maambukizi na kuzuia yasisambae sehemu nyingine ya mwili. Majipu ya fizi hutokea pale bakteria wanapotengeneza maambukizi kati ya fizi na meno, na hii ni matokeo ya mabaki ya vyakula kukwama sehemu hizo. Majipu ya fizi hutumia muda kujitengeneza na mara nyingi hutokea kwa watu wenye magonjwa ya fizi ya muda mrefu. Majipu ya meno hutokea kwenye ncha ya mzizi wa jino na hutokea pale mishipa fahamu inapoelekea kufa au imekufa kabisa. Jipu ka...

KISUKARI NA AFYA YA KINYWA NA MENO

KISUKARI NA AFYA YA KINYWA NA MENO Kisukari kina athari kwa mwili mzima, fizi na meno yakiwamo pia. Athari huwa kubwa zaidi na mbaya kama sukari haijadhibitiwa na kufanya mwili uwe katika ugumu wa kudhibiti maabukizi. Sukari inapokua haijadhibitandoiwa hufanya mtu awe na utando mwingi wa bakteria katika meno na kumfanya awe katika hatari zaidi ya kupata magonjwa ya kinywa na meno kuliko mtu asiye na kisukari au ambaye sukari yake imedhibitiwa. Utando huo katika meno unaweza kusababisha meno kutoboka na pia magonjwa ya fizi  ambayo kwa kitaalamu huitwa "gingivitis"  na periodontitis". Utando katika meno (Dental Plaque) Gingivitis ni hatua ya mwanzo kabisa ya magonjwa ya fizi ambayo husababishwa na uwepo wa utando wa bakteria katika meno. Dalili zake za mwanzo ni pamoja na kutoka damu kwenye fizi na fizi kuwa nyekundu na hata kuvimba. Kwa mtu mwenye kisukari ni ngumu kwa mwili kudhibiti utengenezwaji wa utando huo katika meno, hii ndio sababu hasa ya watu we...

AFYA NA USAFI WA KINYWA KWA WATOTO

AFYA NA USAFI WA KINYWA KWA WATOTO Afya njema ya mtoto ni jukumu la mzazi, afya ya kinywa ni kati ya sehemu muhimu ya afya ya mtoto kwa ujumla. Matunzo ya meno na fizi za mtoto huanza na mzazi mwenyewe. Matunzo mazuri ya meno kwa watoto huwasaidia kuwa na afya njema ya kinywa baadae na hupunguza nafasi ya kupata magonjwa ya kinywa wakiwa wakubwa kwa kuwa wanakuwa wametengenezewa mazingira, uwezo na ufahamu wa jinsi ya kutunza meno na umuhimu wa kufanya hivyo. Usafi wa Kinywa kwa Watoto Wachanga.   Watoto huzaliwa meno yakiwa tayari yamekwisha tengenezwa lakini huwezi kuyaona kwa sababu yanakua ndani ya fizi. Meno huanza kujitokeza nje ya fizi mtoto akiwa na umri kuanzia miezi 6 lakini ni vizuri kuanza usafi wa kinywa kwa mtoto hata kabla meno hayajaanza kutoka kwani "kwenye fizi safi na zenye afya huja meno safi na yenye afya". Futa fizi za mtoto kwa kitambaa safi kila baada ya kumlisha, hii husaidia kuondoa bakteria wanaosababisha meno kuoza. Pale meno...

USAFI WA ULIMI

USAFI WA ULIMI Tofauti na meno, ulimi una uso ambao sio laini na hutengeneza mazingira mazuri kwa vijidudu (bakteria) kuishi na kustawi au kuzaliana. Ulimi huwa na vijidudu wengi ukilinganisha na meno na hii husababisha harufu mbaya ya kinywa. Kama huna matatizo ya meno au fizi basi bakeria waliopo kwenye ulimi ndio sababu kubwa ya harufu mbaya ya kinywa. Jinsi Ya Kusafisha Ulimi Ukiwa umesafisha meno yako kwa usahihi, umakini wa usafi unatakiwa uelekezwe kwenye ulimi.Kusafisha ulimi husaidia kuondoa bakteria katika maeneo yote ya ulimi. Sehemu ya mbele ya ulimi huwa safi mara nyingi lakini sehemu ya nyuma ni muhimu kusafishwa. Kuna vifaa maalumu vya kusafishia ulimi ambavyo huitwa "tongue cleaner" vimetengenezwa madhubuti kwa ajilin hiyo lakini vikikosekana, mswaki unaweza ukasaidia. Ukiwa unasafisha ulimi, anza kwa kuweka kiasi kidogo cha dawa ya meno kwenye mswaki na uanze kusafisha ulimi kwa kuanzia nyuma kwenda mbele ukitumia presha ndogo na kama ukian...

SARATANI YA KINYWA

  SARATANI YA KINYWA Saratani ni ukuaji wa seli za mwili usiodhibitiwa ambao hupelekea kuvamia tishu za jirani na kuziharibu.  Saratani ya kinywa hutokea kama kidonda au ukuaji wa tishu usiopotea. Saratani ya kinywa hujumuisha saratani ya midomo (lips), ulimi, mashavu, chini ya ulimi, taya ya juu, na  koo. saratani ya kinywa inaweza kuhatarisha maisha isipogundulika na kutibiwa mapema. Saratani ya chini ya ulimi Saratani ya mdomo Saratani ya ulimi DALILI ZA SARATANI YA KINYWA. Uvimbe kwenye maeneo mbalimbali ya kinywa Kutokwa na damu katika kinywa kusikokua na sababu Kupata ganzi, kutohisi chochote katika kinywa na maumivu wakati wa kugusa eneo lolote la kinywa, uso au shingo Uwepo wa vidonda kwenye kinywa uso au shingo ambavyo huvuja damu kwa urahisi na kutopona kwa wiki mbili au zaidi. Maumivu ya sikio Kutoweza kula, kuongea na kuchezesha taya au ulimi Kupungua uzito kwa ghafla Ukiwa na dalili hizi tafadhali onana na Daktari wa kinywa na meno ...