Skip to main content

Posts

Showing posts from April, 2020

MFUNGO NA AFYA YA KINYWA NA MENO

       Watu wengi wanatokea kusahau kufanya usafi wa kinywa na meno wakiamini kuwa hakuna tatizo litawapata katika kipindi cha mfungo. Kuhakikisha usafi wa kinywa na meno utasaidia kupunguza harufu mbaya ya kinywa na kinywa kuwa kikavu. NINI HUTOKEA UKIWA UMEFUNGA? Kufunga husababisha kuongezeka kwa kampaundi za madini ya sulphur katika kinywa na husababisha harufu mbaya ya kinywa. Watu wengi wanaamini kuwa kufunga husaidia kutibu magonjwa ya fizi, hii sio kweli. Kuongezeka kwa kampaundi za madini ya sulphur huenda sambamba na kupungua kwa mtiririko wa mate katika kinywa ambayo husababisha kutengenezwa kwa matabaka ya uchafu katika meno kitu ambacho moja kwa moja hupelekea matatizo ya fizi na meno kutoboka. JINSI YA KUTUNZA AFYA YA KINYWA NA MENO KIPINDI CHA MFUNGO. Changamoto nyingi za afya ya kinywa na meno huwepo kipindi cha mfungo. Wengi wamezoea harufu mbaya ya kinywa katika kipindi cha mfungo na huwa wanahisi ni jambo la kawaida. Fanya mamb...

MATE NA MATUMIZI YAKE KATIKA KINYWA.

  Mate yana kazi kubwa na muhimu katika kuimarisha afya kinywa na meno. Hutokana na mfumo wa damu na hivyo huwa kama mkondo wa damu katika kinywa. Hii humaanisha kuwa kama ilivyo kwa damu, mate pia hufanya kazi kubwa katika kuimarisha na kulinda afya ya tishu laini na ngumu katika kinywa. Mtiririko wa mate ukipungua katika kinywa, matatizo kama kuoza kwa meno na vidonda vya mdomoni huanza kujitokeza. Kutafuna ni njia mojawapo ambayo huamsha mtiririko wa mate katika kinywa, husababisha misuli kugandamiza tezi za mate ambazo huzalisha mate. Kazi za mate ni pamoja na; Kuondoa mabaki ya vyakula yaliyoganda katika meno na fizi Kulainisha na kukivunja chakula ili kurahisisha kumeza Kusaidia kuimarisha ladha Kulinda dhidi ya maradhi yanayoweza kushambulia meno na tishu za kwenye kinywa Kufanya uso wa meno kuwa imara kwa kupakaza madini ya calcium, flouride na phosphate katika meno. Pamoja na kulinda na kuimarisha afya ya kinywa, mate yanaweza kuwa na viashiria vya afya...

MATIBABU YA KUSAFISHA MIZIZI YA MENO (ROOT CANAL)

  Kama una jino lililoharibika sana, kuoza au lenye maambukizi (infection), daktari wa meno anaweza akashauri matibabu ya kusafisha mizizi au root canal. Matibabu ya kusafisha mizizi ya jino yanatumika kuokoa jino pale inapohitajika badala ya kulitoa. Nini Hufanyika katika matibabu ya kusafisha mizizi ya jino? Jinsi jino lilivyo kwa muonekano wa ndani. Jino huwa na nafasi ndani yake ambayo huwa na mishipa ya fahamu na damu ambayo hulifanya jino liwe hai. Sehemu hii inaweza kupata maambukizi kama; Una tundu kwenye jino ambalo ni kubwa sana Matibabu ya muda mrefu ambayo yanaweza kusababisha matatizo kwa sehemu hii. Jino likivunjika au kupasuka Ajali yoyote kwenye jino Ukiwa na moja ya matatizo hayo na yasitibiwe, jino hupata maambukizi na kusababisha maumivu makali na wakati mwingine uvimbe ambao husababishwa na jipu linaloota kwenye ncha ya mzizi wa jino. Maambukizi haya yanaweza kusababisha kupoteza jino kwa sababu bacteria wanaosababisha maambukiz...

KUTOBOA MIDOMO (ORAL PIERCINGS)

Kutoboa mwili kumekua kitu maarufu siku za karibuni na imekua kama njia ya kujielezea na kujitambulisha. Kutoboa midomo kunaweza kuonekana ni kitu kizuri na cha kupendeza lakini kinaweza kuleta madhara makubwa kwa mwili na afya. Hii ni kwa sababu kinywa kina vijududu vingi sana ambavyo vinaweza kusababisha maambukizi na kuvimba hasa baada ya kutoboa sehemu za kinywa na midomo.  Kama umetoboa ulimi, mashavu, midomo (lips) na kilimi (sehemu ya nyuma kabisa ya koo), hii inaathiri sana kuongea, kutafuna na pia kumeza, vilevile inaweza ikasababisha; Maambukizi, maumivu na kuvimba. Kwa sababu ya uwingi wa bakteria katika kinywa, kutoboa sehemu za kinywa kunaweza sababisha maambukizi ambayo huwa pamoja na maumivu na kuvimba. Kuvimba kwa ulimi au sehemu aya nyuma ya koo kunaweza sababisha kukosa pumzi na hata kupoteza maisha. Kuharibika kwa meno na fizi Mzio au Allergy Kuharibika kwa mishipa ya fahamu. Hii ni hasa kwa kutoboa ulimi. kunaweza kusababisha kuharibika kwa miship...

HOMONI NA AFYA YA KINYWA NA MENO; JAMBO AMBALO KILA MWANAMKE ANAFAA KULIFAHAMU

                        Uzito, mhemko (mood) na afya ya kinywa na meno. Kuna kitu kimoja ambacho kinaendesha hivi vitu vyote, nacho ni homoni. Unaweza ukajiuliza ni vipi homoni zinauhusiano na afya ya kinywa na meno kwa mwanamke, hii ndio sababu; Homoni nyingi za kike (estrogen na progesterone) zikiwa katika kiwango kikubwa husababisha kuongezeka kwa mtiririko wa damu katika fizi, hii husababisha fizi kuwa sensitive na kuovereact kwa kitu chochote kinachoweza kuziirritate. Wanawake huwa ni sensitive kwa utando unaokua kwenye meno hasa wakati kiwango cha homoni zao kipo juu. Hali hiyo hupelekea fizi kuvimba na kuanza kutoa damu, hali hii isipotibiwa hupelekea ugonjwa kushika kasi na kuharibu mfupa unaoshikilia meno na kupeleka meno kulegea na kutoka. Homoni za mwili ni maisha ila magonjwa ya fizi yanaweza kuzuiwa na kutibiwa katika hatua za mwanzo kabisa. Nini hasa mwanamke anatakiwa kufanya? Anza kuzingatia na kuhakikis...

VIFAA VYA KULINDA KINYWA (MOUTHGUARDS)

MOUTH GUARDS                   Hebu fikiria kama ghafla umepoteza meno yako, tabasamu, kuongea na kula kutaathiriwa kwa kiwango kikubwa sana. Kujua jinsi ya kulinda meno na mdomo hasa wakati wa michezo ni jambo la muhimu sana. Mouthguards husaidia kulinda meno na midomo pale ambapo kuna nguvu inayoweza kupelekea ajali au kuumia kwa meno na midomo. Meno ya juu ya mbele yapo katika hatari kubwa sana ya kuumia kwa sababu yapo nje na yamesogea mbele kidogo ukilinganisha na meno ya chini. Wakati gani utumie Mouthguards? Linapofika suala la kulinda mdomo, mouthguards inatakiwa iwe kati ya vitu muhimu katika shughuli zote za michezo kuanzia mtu akiwa na umri mdogo. Kwa watoto ni muhimu sana kwa sababu michezo yao mingi huhusisha kugusana, kujigonga na kuanguka. Aina za Mouthguards Mouthguards hutengenezwa na madaktari wa meno baada ya kuchukua kipimo cha mdomo ambacho huitwa impression. Pia ku...