Skip to main content

TUJIFUNZE JINSI YA KUSAFISHA KINYWA

Usafi wa kinywa ni muhimu sana kwa ajili ya utunzaji wa meno yetu, kujilinda dhidi ya magonjwa mbalimbali ya kinywa, harufu mbaya ya kinywa na kutoboka kwa meno. Kwa usafi wa kinywa vinahitajika vitu viwili muhimu;
  • Dawa ya meno yenye madini ya floridi kwa kiwango kilichopendekezwa na madaktari wa meno ambacho ni (1450-1500ppm ya F-)
  • Mswaki wenye brashi laini  iliyopendekezwa na madaktari wa meno.
JINSI YA KUSAFISHA MENO
Weka dawa ya meno katika mswaki wako kiasi cha ukubwa wa punje ya kunde, kisha pakaza dawa ya meno katika meno yako kwa kila upande wa meno ( nje, ndani na upande wa kutafunia).

Ifuatayo ni michoro na maelezo yanayoonesha jinsi ya kusafisha kinywa kwa utaratibu unaofaa;


1. Weka mswaki wako kwenye meno kama picha namba moja inavyoonesha, brashi ya mswaki ikiwa imegusa fizi pamoja na meno

2. Pitisha mswaki wako katika pande ya nje ya meno kwa mwendo wa mzunguko ukianzia kushoto kwenda kulia kwa meno ya juu kisha vivo hivyo kwa meno ya chini kwa utaratibu bila kutumia mkandamizo mkubwa kuepuka kuumiza fizi.

3. Tumia mwendo wa kwenda mbele na kurudi nyuma ukiwa unasafisha upande wa ndani wa meno ya nyuma

4. Simamisha wima mswaki wako na tumia mwendo wa juu na chini kusafisha sehemu ya ndani ya meno ya mbele

5. Safisha upande wa kutafunia wa meno kwa kutumia mwendo wa mbele na nyuma.  

Baada ya kumaliza kusafisha meno ni muhimu kusafisha ulimi ili kuzuia harufu mbaya ya kinywa. Pia tunashauriwa kutotema povu la dawa ya meno na kutotumia maji mengi kusuuza kinywa ili kuacha madini ya floridi katika meno kwa ajili ya kuyatunza meno yetu.

Kumbuka kubadilisha mswaki kila baada ya miezi mitatu au pale brashi ya mswaki inapoisha.

 Kusafisha meno ni sehemu tu ya kukamilisha utunzaji wa afya ya kinywa na meno, yafuatayo ni mambo zaidi ya kuzingatia ili kukamilisha utunzaji wa afya ya kinywa na meno; 

  • Safisha kinywa na meno angalau mara mbili kwa siku, asubuhi unapoamka na jioni kabla ya kulala ili kuondoa mabaki ya chakula na utando ambao unaweza kusababisha magonjwa ya fizi na meno kuoza.

  • Kula mlo kamili na punguza matumizi ya vyakula na vinywaji vyenye sukari

  • Tembelea daktari wa meno mara kwa mara kwa ajili ya ushauri wa afya ya kinywa na matibabu pale tatizo litakapoonekana.

     

    Video inayoonesha jinsi ya kupiga mswaki kwa utaratibu unaofaa.

    https://youtu.be/xm9c5HAUBp


Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

HOMONI NA AFYA YA KINYWA NA MENO - VITU AMBAVYO KILA MWANAMKE ANAPASWA KUJUA

 HOMONI ZA KIKE NA AFYA YA KINYWA NA MENO Uzito. Hisia, Mahitaji ya kimwili(sex drive). Afya ya kinywa na meno. Ni vitu ambavyo vinaweza kufanya afya yako ya mwili ikabadilika. Utashangazwa kujua jinsi mabadiliko ya homoni zako yanaweza kukufanya uwe katika hatari ya kupata magonjwa ya fizi. Sababu ni hii. Uwepo wa homoni nyingi za kike katika mwili wako unasababisha damu nyingi kutiririka katika fizi zako na kuzifanya ziwe sensitive na kuoverreact kwakitu chochote kitakachozikera(irritate). Wanawake wapo sensitive na uwepo wa uchafu katika meno yao pale ambapo homoni zao katika mwili zipo juu, hii  husababisha fizi kuvimba na kutoka damu na kama zisipotibiwa hupelekea kupoteza mfupa unaoshikilia meno na kupelekea meno kupotea. Homoni ni maisha na ni kitu kisichoepukika ila magonjwa ya fizi yanaweza kuzuiwa na kutibika katika hatua zake za mwanzo. Sasa nini kifanyike? Anza kwa kuwa makini na afya ya kinywa chako katika vipindi vitano katika maisha yako. 1. Balehe Mabadiliko ya...

UJUMBE SIKU YA AFYA YA KINYWA NA MENO DUNIANI 2025

 

PLASTIC FREE SMILES PROJECT 2023-2024

  Plastic Free Smiles project is an environmental and oral health project designed by Dr. Winfred Mgaya under the umbrella of Tanzania Oral Health Foundation. The project aims to raise awareness on the effects of plastic pollution to the environment specifically caused by plastic toothbrushes and advocating on the adoption of eco-friendly toothbrushes to reduce the plastic pollution caused by plastic toothbrushes. The project is structured to have two phases that will start from November 2023 to April 2024 and May 2024 to November 2024. The project includes physical meetings with target groups as well as online and social media campaigns OBJECTIVES The objective of the advocacy campaign is to raise awareness of the environmental impact of plastic toothbrushes while encouraging people to make the switch to eco-friendly toothbrushes. Specifically, the objectives are: 1. To educate the public on the harmful effects of plastic toothbrushes on the environment. 2. To promote t...