Skip to main content

NINI HUSABABISHA MENO KUOZA?

KUOZA KWA JINO NI NINI?

 

 

Kuoza kwa jino ni kuharibika kwa jino ambako hutokea pale vijidudu au bakteria waliopo mdomoni wanapotengeneza kemikali (asidi) ambayo huharibu jino na kusababisha vijishimo kwenye jino. Vishimo hivyo visipotibiwa vinaweza kusababisha maambukizi (infection), maumivu hata kupotea kwa jino.

Jino lina matabaka makuu matatu

  • Tabaka la nje ambalo huitwa enameli (enamel)

  • Tabaka la kati liitwalo dentini (dentin)

  • Tabaka la ndani liitwalo fofota/tishu (pulp)

Matabaka mengi yakiharibika ndivyo tatizo linapokua kubwa zaidi.

 

NINI HUSABABISHA MENO KUOZA?

 Vijidudu/bakteria na vyakula vyenye asili ya sukari vinaweza kusababisha meno kuoza. Kuna tabaka lenye mnato ambalo huwa linatengenezwa kwenye meno na fizi ambalo kwa kitaalamu huitwa "plaque". Tabaka hili huwa linahifadhi vijidudu au bakteria ambao hutumia sukari kama chakula chao. Bakteria wakiwa wanatumia sukari kama chakula chao hutengeneza kemikali (asidi), asidi hiyo ndiyo inayoshambulia meno na kuyafanya yatoboke. Mchakato huu wote hutokea dakika 20 au zaidi baada ya kula chakula chenye sukari.

 

 Vitu ambavyo vinaweza kuchangia upate kutoboka kwa meno yako ni;

  • Kutosafisha meno mara kwa mara angalau mara mbili kwa siku na kutomwona daktari wa meno mara kwa mara angalau mara moja kwa kila miezi sita kwa ajili ya usafi wa kinywa na matibabu.

  • Kutumia vyakula vyenye sukari mara kwa mara ambavyo bakteria hutumia kama chakula na kuzalisha asidi ambayo husababisha meno kuoza.

  • Kutopata madini ya floridi kwa kiasi cha kutosha. Floridi husaidia kuzuia kuoza kwa meno kwa kuyafanya imara dhidi ya asidi inayotengenezwa na bakteria. Tunaipata floridi ya kutosha katika dawa za meno zenye viwango vilivyothibitishwa na wataalamu wa afya ya meno

  • Kutokuwa na mate ya kutosha kinywani. Mate husaidia kusafisha asidi itengenezwayo na bakteria. Kuna magonjwa ambayo husababisha uzalishwaji mdogo wa mate, ni vyema kuonana na wataalamu kwa ushauri na msaada zaidi hasa kwa watu wenye midomo mikavu.

  • Ugonjwa wa kisukari

  • Uvutaji wa sigara

Comments

Popular posts from this blog

HOMONI NA AFYA YA KINYWA NA MENO - VITU AMBAVYO KILA MWANAMKE ANAPASWA KUJUA

 HOMONI ZA KIKE NA AFYA YA KINYWA NA MENO Uzito. Hisia, Mahitaji ya kimwili(sex drive). Afya ya kinywa na meno. Ni vitu ambavyo vinaweza kufanya afya yako ya mwili ikabadilika. Utashangazwa kujua jinsi mabadiliko ya homoni zako yanaweza kukufanya uwe katika hatari ya kupata magonjwa ya fizi. Sababu ni hii. Uwepo wa homoni nyingi za kike katika mwili wako unasababisha damu nyingi kutiririka katika fizi zako na kuzifanya ziwe sensitive na kuoverreact kwakitu chochote kitakachozikera(irritate). Wanawake wapo sensitive na uwepo wa uchafu katika meno yao pale ambapo homoni zao katika mwili zipo juu, hii  husababisha fizi kuvimba na kutoka damu na kama zisipotibiwa hupelekea kupoteza mfupa unaoshikilia meno na kupelekea meno kupotea. Homoni ni maisha na ni kitu kisichoepukika ila magonjwa ya fizi yanaweza kuzuiwa na kutibika katika hatua zake za mwanzo. Sasa nini kifanyike? Anza kwa kuwa makini na afya ya kinywa chako katika vipindi vitano katika maisha yako. 1. Balehe Mabadiliko ya...

UJUMBE SIKU YA AFYA YA KINYWA NA MENO DUNIANI 2025

 

PLASTIC FREE SMILES PROJECT 2023-2024

  Plastic Free Smiles project is an environmental and oral health project designed by Dr. Winfred Mgaya under the umbrella of Tanzania Oral Health Foundation. The project aims to raise awareness on the effects of plastic pollution to the environment specifically caused by plastic toothbrushes and advocating on the adoption of eco-friendly toothbrushes to reduce the plastic pollution caused by plastic toothbrushes. The project is structured to have two phases that will start from November 2023 to April 2024 and May 2024 to November 2024. The project includes physical meetings with target groups as well as online and social media campaigns OBJECTIVES The objective of the advocacy campaign is to raise awareness of the environmental impact of plastic toothbrushes while encouraging people to make the switch to eco-friendly toothbrushes. Specifically, the objectives are: 1. To educate the public on the harmful effects of plastic toothbrushes on the environment. 2. To promote t...