Skip to main content

NI DAWA IPI YA MENO NZURI KUTUMIA?

AINA ZA DAWA ZA MENO

 Zipo aina nyingi za dawa za meno, aidha, zote zina muunganiko wa madini na kemikali ambazo huzuia meno kuoza, harufu mbaya ya kinywa na kuimarisha afya ya fizi. Ni muhimu kuhakiki ubora wa dawa ya meno unayoitumia kwa kupitia ushauri wa madaktari wa meno au wataalamu waliobobea katika afya ya kinywa na meno kuepuka kutumia dawa za meno zisizo sahihi.


DAWA ZA MENO ZENYE MADINI YA FLORIDI

 Tafiti zimeonesha kwamba kushuka kwa ongezeko la watu wenye meno mabovu katika nchi zilizoendelea kwa miaka 30 iliyopita, imechangiwa kwa kiasi kikubwa na matumizi ya dawa za meno zenye madini ya floridi.Tafiti zimeonesha kuwa muunganiko wa floridi na madini mengine unaweza kuzuia kutoboka kwa meno na kuyafanya meno yawe imara.


KIWANGO CHA FLORIDI KATIKA DAWA YA MENO

Kiwango cha floridi katika dawa za meno huandikwa katika kasha la dawa ya meno ikiwa na alama za (% w/v) , (% w/w) au (ppm F-). Kiwango kinachoshauriwa na madkatari wa meno ni 1000-1500 ppm F-. Zipo dawa za meno zenye viwango zaidi ya hivyo lakini hutolewa kwa maelekezo maalumu ya daktari wa meno.


DAWA ZA MENO KWA WATOTO.

Kwa kuwa watoto chini ya umri wa miaka 6 wanaweza kumeza dawa ya meno wakati wa kusafisha meno, dawa ya meno yenye madini ya floridi kwa kiwango cha 1450-1500 ppm F- yanaweza kuwaletea watoto meno yenye rangi na matatizo ya tumbo pia. Hivo basi wataalamu wa afya ya kinywa na meno wanashauri watoto watumie dawa za meno zenye viwango vya chini vya madini ya floridi ambavyo ni 500-600 ppm F-, na kusimamiwa wakati wa kupiga mswaki.

Comments

Popular posts from this blog

HOMONI NA AFYA YA KINYWA NA MENO - VITU AMBAVYO KILA MWANAMKE ANAPASWA KUJUA

 HOMONI ZA KIKE NA AFYA YA KINYWA NA MENO Uzito. Hisia, Mahitaji ya kimwili(sex drive). Afya ya kinywa na meno. Ni vitu ambavyo vinaweza kufanya afya yako ya mwili ikabadilika. Utashangazwa kujua jinsi mabadiliko ya homoni zako yanaweza kukufanya uwe katika hatari ya kupata magonjwa ya fizi. Sababu ni hii. Uwepo wa homoni nyingi za kike katika mwili wako unasababisha damu nyingi kutiririka katika fizi zako na kuzifanya ziwe sensitive na kuoverreact kwakitu chochote kitakachozikera(irritate). Wanawake wapo sensitive na uwepo wa uchafu katika meno yao pale ambapo homoni zao katika mwili zipo juu, hii  husababisha fizi kuvimba na kutoka damu na kama zisipotibiwa hupelekea kupoteza mfupa unaoshikilia meno na kupelekea meno kupotea. Homoni ni maisha na ni kitu kisichoepukika ila magonjwa ya fizi yanaweza kuzuiwa na kutibika katika hatua zake za mwanzo. Sasa nini kifanyike? Anza kwa kuwa makini na afya ya kinywa chako katika vipindi vitano katika maisha yako. 1. Balehe Mabadiliko ya...

UJUMBE SIKU YA AFYA YA KINYWA NA MENO DUNIANI 2025

 

PLASTIC FREE SMILES PROJECT 2023-2024

  Plastic Free Smiles project is an environmental and oral health project designed by Dr. Winfred Mgaya under the umbrella of Tanzania Oral Health Foundation. The project aims to raise awareness on the effects of plastic pollution to the environment specifically caused by plastic toothbrushes and advocating on the adoption of eco-friendly toothbrushes to reduce the plastic pollution caused by plastic toothbrushes. The project is structured to have two phases that will start from November 2023 to April 2024 and May 2024 to November 2024. The project includes physical meetings with target groups as well as online and social media campaigns OBJECTIVES The objective of the advocacy campaign is to raise awareness of the environmental impact of plastic toothbrushes while encouraging people to make the switch to eco-friendly toothbrushes. Specifically, the objectives are: 1. To educate the public on the harmful effects of plastic toothbrushes on the environment. 2. To promote t...