
Magego ya mwisho au wisdom teeth ni meno ya mwisho kabisa kuota katika mdomo na huota kati ya miaka 17 mpaka 25. Meno haya huwa mawili kwa kila taya moja kila upande wa taya na kufanya jumla yake iwe manne. Sio watu wote huota haya magego ya mwisho na hata kam yakiota kwa watu wengi huwa hayajakaa katika mstari kama meno mengine lakini kwa wachache huwa yanaota vizuri kabisa.
Mara nyingi magego ya mwisho huotea ndani ya taya na hayatoki nje na hata kama yakitoka huota vibaya na kusababisha kuoza na hata magonjwa ya fizi hii husababishwa na kuwepo kwa fizi juu ya meno haya ambayo huifadhi vyakula na kusababisha infection na maumivu.
Kwanini magego ya mwisho huota vibaya?
Magego ya mwisho huota vibaya kwasababu hayapati nafasi ya kuota kwa kawaida. Magego ya mwisho huota kati ya miaka 17 mpaka 25, umri ambao mdomo tayari unakua na meno mengi hivyo basi kukosa nafasi ya kuota vizuri na kuishia kuota katika hali ambayo sio ya kawaida (impacted).
Matatizo yanayoweza kuletwa na Magego ya mwisho ambayo hayajaota vizuri.
- Uharibifu kwa meno mengine
- Kutengenezwa kwa kimfuko chenye maji au CYST ambacho kinaweza kuleta athari kwa mfupa na mishipa ya fahamu
- Meno kuoza
- Magonjwa ya fizi
Je kuna ulazima wa kuyatoa magego ya mwisho?
Kwa magego ya mwisho ambayo hayajaota vizuri, ni vizuri kuyatoa ili kuepusha matatizo yanayoweza kutokea baadae kutokana na ukaaji wa magego hayo. Kulingana na sehemu jino lilipo na lilivyoota, magego ya mwisho yanaweza kutolewa katika kliniki ya meno au katika chumba cha upasuaji.
Ahsante sana nimepata kitu
ReplyDelete