KUOZA KWA JINO NI NINI? Kuoza kwa jino ni kuharibika kwa jino ambako hutokea pale vijidudu au bakteria waliopo mdomoni wanapotengeneza kemikali (asidi) ambayo huharibu jino na kusababisha vijishimo kwenye jino. Vishimo hivyo visipotibiwa vinaweza kusababisha maambukizi (infection), maumivu hata kupotea kwa jino. Jino lina matabaka makuu matatu Tabaka la nje ambalo huitwa enameli (enamel) Tabaka la kati liitwalo dentini (dentin) Tabaka la ndani liitwalo fofota/tishu (pulp) Matabaka mengi yakiharibika ndivyo tatizo linapokua kubwa zaidi. NINI HUSABABISHA MENO KUOZA? Vijidudu/bakteria na vyakula vyenye asili ya sukari vinaweza kusababisha meno kuoza. Kuna tabaka lenye mnato ambalo huwa linatengenezwa kwenye meno na fizi ambalo kwa kitaalamu huitwa "plaque". Tabaka hili huwa linahifadhi vijidudu au bakteria ambao hutumia sukari kama chakula chao. Bakteria wakiwa wanatumia sukari kama chakula chao hutengeneza kemikali (asidi), asidi hi...
ELIMU,USHAURI NA MSAADA KUHUSU AFYA YA KINYWA. MAWASILIANO: PHONE; +255716817627, +255743507651 EMAIL; tanzaniaoralhealthfoundation@gmail.com