Skip to main content

KUNG'ARISHA MENO (TEETH WHITENING) - VITU UNAVYOPASWA KUJUA

Kupiga mswaki kwa usahihi ndio njia ambayo inaweza kukufanya uwe na tabasamu zuri na meno yenye mng'ao. Lakini je unawaza kufanya meno yako yawe meupe zaidi? Basi ni vizuri ukajua ukweli kuhusu matibabu haya. Nitaelezea kwa kujibu maswali ambayo huwa yanaulizwa sana kuhusu kufanya meno yawe meupe.

Kwanini Meno yanabadilika rangi?

Kwa muda meno yako yanaweza kubadilika kutoka rangi nyeupe kwenda kwenye rangi iliyofifia kutokana na sababu tofauti ambazo ni;
  1. Vyakula na vinywaji; Kahawa, chai na mvinyo mwekundu ni vinywaji ambavyo vinaleta sana kubadilika kwa rangi ya meno. Vinywaji hivi vina rangi ambayo huganda kwenye tabaka la nje la meno.
  2. Matumizi ya tumbaku na sigara; Vitu viwili vilivyopo kwenye sigara ndivyo hufanya rangi ya meno ibadilike navyo ni lami na nicotine. Lami ni nyeusi kwa asili lakini nicotine hubadilika rangi inapochanganyika na hewa ya oxygen na kuwa njano ambayo huonekana sana kwenye meno ya wavutaji wa sigara.
  3. Umri; Chini ya tabaka gumu kabisa la meno kuna tabaka ambalo ni laini kidogo liitwalo dentine, umri unavyosogea tabaka gumu la juu hupungua na hivyo kupelekea tabaka la dentine kuonekena ambalo lina rangi ya unjano hii ndio sababu wazee wana meno ambayo ni rangi ya njano kidogo.
  4. Madawa. Kuna baadhi ya madawa ambayo hutumika kwa matibabu tofauti husababisha rangi ya meno kubadilika na pia matibabu ya mionzi.
Matibabu ya kufanya meno yawe meupe (whitening) hufanyikaje?

Matibabu ya kufanya meno kuwa meupe hutumia dawa ambazo zina kemikali salama ambazo hufanya meno yawe meupe. Kemikali hizi ni hydrogen peroxide na carbamide peroxide.

Whitening inafanya kazi kwenye meno ya aina yote?

HAPANA. Hii ni sababu pia inayoshauriwa kuongea na daktari wa meno kabla ya kufanya utaratibu huu wa kung'arisha meno. Whitening haifanyi kazi kwenye meno yote yaliyobadilika rangi inategemea na sababu ya kubadilika rangi. Meno yaliyobadilika rangi kwa sababu ya ajali au madawa hayawezi kufanyiwa whitening kabisa.

Ni njia zipi naweza tumia kufanya whitening?
Ni vyema ukaongea na daktari wako wa meno kuhusu kuwhiten meno yako na machaguo yaliyopo ila kuna njia kuu nne ambazo zinatumika kufanya meno yawe meupe nazo ni;
  1. Dawa za meno zinazotumika kung'arisha meno. Dawa hizi huwa na kitu ndani yake ambacho husaidia kufanya meno yawe meupe. Ni vizuri kuzifahamu kabla ya kuzitumia kuepuka athari.
                       Natural Intensive Stain Remover Whitening Toothpaste - Yoomoz
  1. Matibabu ya daktari. Njia hii hutumia dawa maalumu ambayo ina muongozo wa kuitumia na hufanyika katika kliniki ya meno na hufanywa na daktari.
                         Differences Between at Home And In Office Tooth Whitening Procedures
  1. Dawa za kutumia nyumbani. Dawa hizi hutolewa kwa maelekezo ya daktari ila hutumika nyumbani ukiwa unafuatiliwa kwa ukaribu na daktari na huachwa pale tu weupe wa meno unapoonekana 
                     White Smile Home Teeth Bleaching Led Light Whitening Kit - Buy ...Nini athari za whitening?
Baadhi ya watu ambao wametumia bidhaa za kung'arisha meno wamepata athari ya meno kuwa na ganzi na pia kutumia bidhaa hizi kwa muda mrefu husbabisha kupungua kwa tabaka la juu la meno.

Ni vyema kuongea na daktari wako ili kujua njia sahihi na matumizi sahii ya bidhaa za kung'arisha meno


Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

HOMONI NA AFYA YA KINYWA NA MENO - VITU AMBAVYO KILA MWANAMKE ANAPASWA KUJUA

 HOMONI ZA KIKE NA AFYA YA KINYWA NA MENO Uzito. Hisia, Mahitaji ya kimwili(sex drive). Afya ya kinywa na meno. Ni vitu ambavyo vinaweza kufanya afya yako ya mwili ikabadilika. Utashangazwa kujua jinsi mabadiliko ya homoni zako yanaweza kukufanya uwe katika hatari ya kupata magonjwa ya fizi. Sababu ni hii. Uwepo wa homoni nyingi za kike katika mwili wako unasababisha damu nyingi kutiririka katika fizi zako na kuzifanya ziwe sensitive na kuoverreact kwakitu chochote kitakachozikera(irritate). Wanawake wapo sensitive na uwepo wa uchafu katika meno yao pale ambapo homoni zao katika mwili zipo juu, hii  husababisha fizi kuvimba na kutoka damu na kama zisipotibiwa hupelekea kupoteza mfupa unaoshikilia meno na kupelekea meno kupotea. Homoni ni maisha na ni kitu kisichoepukika ila magonjwa ya fizi yanaweza kuzuiwa na kutibika katika hatua zake za mwanzo. Sasa nini kifanyike? Anza kwa kuwa makini na afya ya kinywa chako katika vipindi vitano katika maisha yako. 1. Balehe Mabadiliko ya...

VINA SABA NA AFYA YA KINYWA NA MENO

       Je vinasaba vinaweza kutabari uwezekano wa kupata magonjwa ya fizi na meno kutoboka? Je, magonjwa ya kutoboka meno na fizi hurithishwa? Jibu kwa sasa ni HAPANA. Magonjwa ya meno kutoboka na fizi yanachangiwa sana na mazingira na mitindo ya maisha na sio vina saba au kurithishwa. Usafi wa kinywa, vitu unavyokula, matumizi ya tumbaku yana mchango mkubwa sana katika kupata magonjwa ya fizi na meno kutoboka. Vifaa vya uchunguzi vinavyotumiwa na daktari pamoja na picha za xray ndivyo husaidia kujua hali ya afya yako ya kinywa kwa sasa na kutabiri hali katika siku za mbeleni. Chukua hatua sasa katika kuzuia magonjwa ya fizi na meno kutoboka kwa kufanya yafuatayo Piga mswaki angalau mara mbili kwa siku Safisha sehemu ya katikati ya meno yako kwa kutumia uzi maalum au floss Kula chakula bora na chenye afya na punguza matumizi ya vyakula vyenye sukari Fanya uchunguzi wa afya ya kinywa angalau mara mbili kwa mwaka

UJUMBE SIKU YA AFYA YA KINYWA NA MENO DUNIANI 2025