Skip to main content

Posts

Showing posts from June, 2020

MAGEGO YA MWISHO - (WISDOM TEETH)

       Magego ya mwisho au wisdom teeth ni meno ya mwisho kabisa kuota katika mdomo na huota kati ya miaka 17 mpaka 25. Meno haya huwa  mawili kwa kila taya  moja kila upande wa taya na kufanya jumla yake iwe manne. Sio watu wote huota haya magego ya mwisho na hata kam yakiota kwa watu wengi huwa hayajakaa katika mstari kama meno mengine lakini kwa wachache huwa yanaota vizuri kabisa. Mara nyingi magego ya mwisho huotea ndani ya taya na hayatoki nje na hata kama yakitoka huota vibaya na kusababisha kuoza na hata magonjwa ya fizi hii husababishwa na kuwepo kwa fizi juu ya meno haya ambayo huifadhi vyakula na kusababisha infection na maumivu. Kwanini magego ya mwisho huota vibaya? Magego ya mwisho huota vibaya kwasababu hayapati nafasi ya kuota kwa kawaida. Magego ya mwisho huota kati ya miaka 17 mpaka 25, umri ambao mdomo tayari unakua na meno mengi hivyo basi kukosa nafasi ya kuota vizuri na kuishia kuota katika hali ambayo sio ya kawaida (impacted)....

WASIWASI WA MATIBABU YA MENO: NJIA 3 ZA KUSAIDIA KUONDOA WASIWASI WA MATIBABU

              Kama umekua ukipata wasiwasi wa kwenda kumuona daktari wa meno, jua kwamba hauko peke yako. Pengine unahisi utapata maumivu au hujui nini daktari atafanya kulingana na atakachokiona. Sababu za wasiwasi zinaweza kuwa; Kutokuwa na taarifa sahihi kutoka kwa daktari, kupata maumivu baada ya matibabu au mawazo hasi kuhusu matibabu ya meno. Kwa sababu yoyote ile, timu nzuri ya madaktari itasaidia kuhakikisha afya yako ya kinywa na meno pamoja na kimawazo inakuwa nzuri. Unavyochelewa zaidi kumuona daktari wa meno ndivyo unavyokua kwenye hatari ya kupata matatizo makubwa zaidi na kusababisha matibabu yawe magumu zaidi. Mathalani, kumuona daktari wa meno mapema kutasaidia kufanya matibabu yawe rahisi na muda mfupi. Zifuatazo ni njia ambazo unaweza kuzitumia ukiwa unaenda kumuona daktari wa meno ili kupunguza wasiwasi na kufanya uwe na tabasamu lenye uangavu. Ongea Mtu yoyote mwenye wasiwasi, akiongea hufanya mabadiliko makubwa kwa hisi...

MAFUA NA KIKOHOZI; MAMBO MATANO UNAYOPASWA KUFANYA UKIWA NA MAFUA NA KIKOHOZI

        Ukiwa na mafua na au kikohozi, kuweka mwili wako sawa na katika hali ya usafi ni jambo la msingi na muhimu na hii inahusisha usafi wa kinywa pia. Zifuatazo ni njia rahisi ambazo unaweza kuzitumia ili kuhakikisha afya ya kinywa na meno inabaki kuwa nzuri na imara wakati unaumwa. Zingatia Usafi mzuri Ukiwa unaumwa  mafua na kikohozi ni vyema kuziba mdomo na pua wakati wa kukohoa na kupiga chafya pia usisahau kuhakikisha afya ya kinywa chako inazingatiwa. Tafiti zinaonesha kwamba virusi vya mafua vina uwezo wa kukaa sehemu yenye unyevu kwa takribani masaa 72. Hivyo basi ni vyema kutoshirikiana kutumia mswaki mmoja kwa watu wawili pia ni vizuri kubadilisha mswaki mara baada ya kupona mafua ingawa asilimia za kupata mafua kutoka kwenye mswaki ni ndogo lakini ni vyema kuchukua tahadhari. Tumia dawa ambazo hazina sukari Kama inavyojulikana kwamba sukari ndio chanzo kikubwa cha meno kuoza, hivyo basi kutumia dawa ambazo zina sukari zinaweza kuleta at...